tiko
tiko
Matatizo
katika uzalishaji wa mbegu za kiume inahusiana na kutokuwepo kwa mbegu
za kiume kwenye manii au uwepo wa mbegu kidogo sana katika manii.
Mbegu za kiume huwa zinachunguzwa kwa kutumia kifaa maalum au darubini
katika maabara, kwa kawaida mwanaume ili aweze kumpa mwanamke mimba
anatakiwa atoe kiasi cha mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia
tatu hamsini kwa tendo, chini ya milioni ishirini huwezi kumpa mimba
mwanamke.
Endapo kiwango cha mbegu zitakuwa kidogo kitaalam hali hiyo huitwa
‘Oligospermia’ na kama huna kabisa mbegu hali hiyo huitwa
‘Azoospermia.Dalili za kutokuwa na mbegu za kiume
Hakuna dalili za moja kwa moja kusema kwamba utaumwa kitu fulani, lakini
dalili zifuatazo huambatana na tatizo hili; kwanza ni kukaa katika
mahusiano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja lakini mwenzi wako
hapati mimba, kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa uume kukosa nguvu’ Low
sex Drive’ na ukisimama unashindwa kuendelea na kumalizia tendo
‘Erectile dysfunction’ pamoja na kuwahi kumaliza tendo la ndoa.
Maumivu na uvimbe wa korodani, kupungua kwa vinyweleo na ndevu kutoota
pia ni dalili inayoashiria matatizo ya uzazi kwa mwanaume kwani ni
ishara ya upungufu wa Kromozomu au homoni za kiume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.
Wakati gani wa kumuona daktari?
Endapo umekaa na mwenzio mwaka mmoja au zaidi, mnafanya tendo la ndoa bila kinga yaani kizuizi chochote wakati wa kupangilia ujauzito lakini mimba haipatikani. Kama una matatizo ya nguvu za kiume au unawahi kumaliza tendo la ndoa. Unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au uume unalegea wakati wa tendo pia ni mojawapo ya chanzo.

Unakuwa na maumivu ya korodani au korodani kuvimba, maumivu ya uume na
maumivu wakati wa kukojoa au uwepo wa kivimbe katika uume.
Chanzo cha tatizo
Uzalishaji wa mbegu za kiume unafuatana na ubora wa korodani kama haina tatizo lolote na kiwango bora cha mfumo wa homoni mwilini mwake. Homoni zinadhibitiwa katika ubongo na kuimarisha korodani zizalishe mbegu. Mbegu zikishazalishwa, husafirishwa na mirija midogo sana na laini hadi katika tezi dume’Prostate gland’ ambayo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii.

Matatizo katika mbengu za kiume ni kutokuwepo kwa mbengu
kunakosababishwa na hitilafu kwenye korodani, kuzalisha mbegu zenye
kasoro, mbegu zisizo na kiasi na mbegu chache.
Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi katika korodani na uume na kuumia korodani.
Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi katika korodani na uume na kuumia korodani.
Mishipa ya damu kulalia korodani ‘Variocele’ pia ni mojawapo ya tatizo kubwa la kuziba kwa mirija ya usafirishaji mbegu hizo.
Zipo pia sababu za kimazingira zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume
mfano kemikali za viwandani, rangi za viwandani au majumbani, dawa za
mashambani na za kuua wadudu, mionzi ya X- Ray, kukaa kwenye joto kali,
kuvaa nguo za kubana na kukaa mahali kwa muda mrefu, kupakata kompyuta
‘Lap top’ kwa muda mrefu, matumizi ya sigara, bangi na madawa mengine
ya kulevya kwa muda mrefu na ulevi uliokithiri. Uzito mkubwa wa mwili na
matatizo ya akili.
Uchunguzi
Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya kwa madaktari wa masuala ya uzazi.
Vipimo vya damu kuangalia mwenendo wa mfumo wa homoni mwilini Kipimo cha Ultrasound kuangalia korodani yako kwa ndani.

Uchunguzi hufanyika kisayansi hospitali tu, hakuna vifaa vingine vya
kuchunguza kwa kubahatisha, unatakiwa utolewe damu, na utoe mbengu zako
za kiume baada ya kupumzika kufanya tendo la ndoa angalau kwa siku
tatu.
Matibabu na ushauri
Hufanyika baada ya uchunguzi ambapo daktari atatoa dawa kuzingatia na tatizo lililopo.
Kama hakuna mbegu zipo chache au kuna maumivu au kasoro zozote.Uwepo wa kasoro za viungo vya uzazi pia ni tatizo mfano, uume mfupi, kutokuwa na korodani au kuwa na korodani moja. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment