tiko
tiko
MSANII filamu
za Kibongo, Manaiki Sanga amefungukai kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii
mwenzake, Jacqueline Walper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi
wazazi wake.
Akichezesha taya na Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi
wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.
“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na
hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa
maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema
Manaiki.
Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake
walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment