tiko
tiko
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba leo amewasihi Jumuiya ya Vijana wa CUF(JUVICUF) kusitisha maandamano kama jeshi la polisi lilivyoagiza .
Akizungumza
leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini Dar e s
Salaam, amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu kunaweza
kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi, vifo na
kadhalika.
Alisisitiza
waache kuandamana ingawa dhamira yao ya kuitaka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa upigaji kura kutoka
siku saba hadi 14 ina mantiki kwa Watanzania wote.
JIVICUF
walikuwa waandamane kusisitiza, miongoni mwa mambo mengine, kuhusu
uvunjwaji wa haki za binadamu nchini na dosari za uandikishaji wapiga
kura.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment