tiko
tiko
Utata
umezingira suala la kijana George Mgoba, ambaye amekuwa akijitambulisha
kuwa kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
baada ya habari kuwa alitekwa na baadaye kutupwa kwenye Msitu wa Pugu,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar
es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa,
kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo
hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa
maelezo mengi.
Mgoba amekuwa akihamasisha vijana
wenzake waliohitimu ya JKT kukusanyika jijini Dar es Salaam na
kuandamana hadi kwa Rais ili kumweleza masikitiko yao ya kutopatiwa
ajira baada ya kumaliza mafunzo kama walivyoahidiwa wakati wakienda
kwenye kambi za jeshi hilo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment