tiko
tiko
KIKONGWE Hilda
Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina
katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado
hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo, kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4).
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
“Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela, waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lameck Zenda (22), Pautas Komba (24), Fredy Mende (24), Gerord Ngonyani (27), Odilo Mwingira (21), Shadrack Ngonyani (22), Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Muunganozomba.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka huu.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment