tiko
tiko
BAADA ya
kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi, mwigizaji Jacqueline
Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa hayuko tayari
kuolewa tena.
Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha
yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.
“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema
ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza
sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,”
alisema Jack.
Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa
talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment