tiko
tiko
Shabiki
maarufu wa Michael Jackson ambaye alikuwa ni Mfalme wa Musiki wa Pop
ambaye kwa sasa ni marehemu, ametumia zaidi ya pauni za Uingereza 2000
(sawana shilingi za Tanzania 5,590,621) kuchubua ngozi yake ili kufanana
na mwanamuziki huyo.
Shabiki
huyo Mbrazil, Antonia Gleidson Rodrigues, 32 ambaye amejitangaza kuwa
mtu pekee anayefanana na Michael Jackson kuliko wote nchini Brazil,
amefanyiwa upasuaji ili kufanana na Michael huku akitumia zaidi ya saa 4
kila siku kujifunza kucheza filamu na muziki kama Michael Jackson.
“Gleidson
Jackson”, kama ambavyo hupenda kuitwa, alifanyiwa upasuaji mara ya
kwanza miaka mitano iliyopita, ambapo alirekebishwa pua ili aweze kuimba
sauti ya juu.
Baada
ya upasuaji wa kwanza, mkazi huyo wa Fortalenza, Brazil aliendelea na
mkakati wake wa kufanana na mwanamuziki huyo wa pop kwa kudungwa
tindikali ili kuufanya uso wake kuwa mweupe, pamoja na sindano
zilizofanya maeneo yanayo zunguka macho kubadilika.
Gliedson
ambaye alikuwa mwalimu wa maigizo, alifanyiwa upasuajia ili kuziba
nafasi zilizopo meno yake, kurekebisha kope kwa kuzichora kama
tattoo. Sasa hivi shabiki huyo anakusanya pesa kwa kumuigiza Michael
Jackson ili aweze kulipia upasuaji mwingine zaidi.
Anasema:
“Kama nitamudu gharama, nafikiria kufanyia kazi magego iliniondokane na
mikunjo ya mdomoni – nataka pia kuchonga nyusi. Ningependa pia paji
langu la uso lichorwe (tattoo) na kuchonga pua yangu iwe nyembamba
zaidi.”
Gleidson
alivutiwa kuwa kama Michael Jackson alipokuwa na miaka 19 baada ya
mwanafunzi mwenzake kumwambia anafanana na mkongwe WackoJacko. “Ilikuwa
ngumu, nilitaniwa kwa siku 15. Mwishowe nikanasa – nikaambukizwa.”
Gleidson
anasema kwa sasa alivyo na anavyojitahidi kuwa ni zawadi tosha
anayoweza kumpa supastar Michael ambaye kwa sasa ni marehemu. “Katika
matamasha yangu huwa nnasema hakuna kopi inayoweza kuwa nzuri kama
origino, Pamoja na hayo nitajitahidi kuwa na kufikia vilele vya ubora –
kama Michael”
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment