tiko
tiko
Miezi 14 imepita tangu itolewe hukumu ya
kifungo cha miaka saba kwa waandishi wa habari wawili na mwingine mmoja
kufungwa miaka 10 kwa kosa la kuripoti habari za kichochezi wakiwa
ndani ya Egypt wakati wa machafuko ya kisiasa, leo kuna taarifa nzuri
kuhusu waandishi hao.
Mahakama ya Misri iliagiza kuachiliwa kwa waandishi wa habari wawili wa kituo cha Aljazeera, Baher Mohamed na Mohamed Fahmy waliohukumiwa kwa kosa la kuandika habari za kutetea kundi la Muslim Brotherhood ambacho baadaye kilipigwa marufuku kwenye nchi hiyo.
Mohammed Fahmy na Baher Mohammed wamekaa jela kwa zaidi ya siku 400 kila mmoja na mwenzao raia wa Australia, Peter Greste alirudishwa nyumbani kwao Australia kwa amri ya Rais Fattah el-Sisi,
maamuzi ya Jaji wa Mahakama iliyotoa kibali cha kuachiliwa waandishi
hao yanawaweka huru mpaka siku ya February 23 kwa ajili ya kusilizwa
upya kwa kesi hiyo.
Ndugu na jamaa wa waandishi hao
waliokuwa Mahakamani hapo walipokea kwa furaha taarifa za ndugu zao
kuachiwa, huku masikio na macho yao wakisubiri hukumu itakatotolewa kwa
mara ya pili.
Waandishi wengi duniani walilaumu kitendo cha kufungwa Wanahabari hawa wakidai kuwa ‘wamefungwa kwa hatia ya kutekeleza majukumu yao’.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment