tiko
tiko
SIMULIZI ya
vifo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa ajali ya moto
huko Kipunguni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita inatisha, baada ya
majirani kuanika ushuhuda waliousikia dakika chache kabla ya wapendwa
hao kukata pumzi, Uwazi lina habari kamili.
Nyumba iliyoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu sita.
Katika ajali hiyo, Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpira, mkewe, watoto
wao na wajukuu wawili walifariki kwa moto huo unaodaiwa kutokea kutokana
na hitilafu ya umeme.
Jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Ally alisema siku ya
tukio kulikuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.“Kwa kweli
sijawahi kuona pigo kubwa kwa familia kama hili, huyu ni jirani yetu
aliyeishi nasi kwa upendo wa hali ya juu kabisa. Tofauti na
inavyofahamika kuwa wanajeshi ni wakorofi, marehemu alikuwa mfano wa
kuigwa kwani alikuwa ni mnyenyekevu,” alisema Abdallah.
Waombolezaji wakiwa na simanzi kubwa.
“Jirani yangu ameungua kama kuni, siamini kama hatunaye tena, kweli
jamani watu wazuri hawadumu, huyu baba na familia yake walikuwa mstari
wa mbele katika masuala ya kijamii,” alisema jirani mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Julius.
Kwa pamoja, majirani hao walisema walipofika eneo la tukio baada ya
kusikia vilio kutoka ndani ya nyumba hiyo, walijitahidi kuvunja milango
na madirisha, lakini moshi mkubwa ulikuwa umeshatanda ndani.
“Nilisikia sauti ya mama mara tatu akisema Yesu, Yesu, Yesu, hivyo nguvu
zetu zote zikaelekea upande uliotoka ile sauti, tukiamini wote
watakuwa sehemu moja, lakini kibaya moshi ulikuwa mkubwa sana hivyo
ulituzidi nguvu waokoaji ukizingatia hatukuwa na zana za kisasa za
uokoaji,” alisema jirani mmoja.
Mashuhuda hao walidai baada ya sauti ya mama huyo kunyamaza, hawakusikia
tena chochote hadi baada ya nyumba kuteketea, walipowakuta wanandoa hao
maiti zao zikiwa zimekumbatiana mlangoni.
Walioteketea katika ajali hiyo ni David Mpira (60), Selin Egela (50) (Dada wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya, Lucas Mpira (20), Celina Emmanuel (9) na Pauline Emmanuel (4).
Walioteketea katika ajali hiyo ni David Mpira (60), Selin Egela (50) (Dada wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya, Lucas Mpira (20), Celina Emmanuel (9) na Pauline Emmanuel (4).
Gari la polisi likiwa eneo la tukio.
Mwanafamilia mwingine, Emmanuel Mpira ambaye ni mgonjwa, alikuwa
amejilaza nje kwa sababu ya kukimbia joto wakati moto huo ulipoanza na
kuwateketeza wenzake. Emmanuel alisema kwamba akiwa amelala nje aliuona
moto wa ajabu ukiwaka akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa kuhusiana na ajali hiyo, walililaumu
Shirika la Umeme la Tanesco kwa kitendo chake cha kuwasha na kuzima
umeme kuwa ndicho kilikuwa chanzo kikubwa cha moto huo.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment