tiko
tiko
Ni Jumatatu nyingine ninapokukaribisha msomaji wangu katika ukurasa wetu
huu, tujadiliane na kuzungumza mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa
kimapenzi. Wiki iliyopita, nilihitimisha mada iliyokuwa inazungumzia
mwanamke mzuri anapaswa kuwa na vigezo gani?
Kutokana
na maombi ya wasomaji wangu, nimeamua kuhamia upande wa pili na
kujadili pia sifa za mume au mwanaume bora. Nazungumza na wewe mwanamke
au msichana, hivi umewahi kujiuliza sifa za mwanaume bora ni zipi?
Tukizungumzia mume bora au mwanaume bora, kichwani unajenga picha gani?
WENGI WANADANGANYIKA NA SIFA ZA NJE
Kama tulivyojadili kwenye mada iliyopita kwamba wanaume wengi hudanganyika na sifa za nje za mwanamke, hali iko hivyohivyo kwa wanawake ambao nao ni wepesi sana wa kudanganyika na sifa za nje za mwanaume.

Ukipata nafasi ya kuwasikiliza wanawake juu ya wanaume wanaowapenda,
utashangaa kusikia wakisema kwamba mwanaume bora ni yule mwenye gari la
kifahari, mwenye nyumba, mwenye fedha au mwenye mwili wenye misuli
iliyojengeka vizuri au anayepiga pamba kali.
Wengi wanashindwa kuelewa kwamba sifa hizo za nje hazitoshi kutoa
tathmini ya mwanaume bora na matokeo yake, wanajikuta wakiingizwa kwenye
mitego ya wanaume kwa urahisi. Kwa kuwa wanaume wanajua wanawake
wanapenda nini, siku hizi kuna mtindo mpya wa namna ya kuwanasa
wanawake.
Mwanaume yupo tayari kwenda kuazima gari kwa rafiki yake au kukodisha,
yupo tayari kwenda kuazima nguo kwa rafiki zake na kwenda kuingia madeni
kwa kukopa fedha ili aonekane anazo. Wanaume wanalazimika kudanganya
uhalisia wa maisha yao ili waweze kutimiza haja zao kwa wanawake.
Wengine wanashindwa kujishughulisha katika kazi zinazoweza kuyabadilisha maisha yao na badala yake wanashinda Gym kutanua vifua ili wawanase wasichana warembo!
Wengine wanashindwa kujishughulisha katika kazi zinazoweza kuyabadilisha maisha yao na badala yake wanashinda Gym kutanua vifua ili wawanase wasichana warembo!
VIGEZO VYA MUME BORA VIPO TOFAUTI KABISA
Kama ilivyokuwa kwa sifa na vigezo vya mwanamke bora, kwa upande wa wanaume pia ni hivyohivyo. Sifa za nje pekee hazitoshi kumfanya mtu amjue mwanaume bora ni yupi. Hujawahi kukutana na mwanamke mwenye sifa zote zinazotakiwa akiwa amenasa kwenye penzi la mwanaume ambaye jamii nzima inajiuliza ‘amempendea nini yule? Mbona hawafanani?’

Hujawahi kuona kwamba mwanamke anawakataa wanaume wenye fedha, magari na
kila kitu lakini anamng’ang’ania mwanaume ambaye jamii inamtafsiri
kwamba hana sifa wala vigezo vya kuitwa mume au baba bora?
Mwonekano wa nje, fedha, magari, majumba na vitu vingine kama hivyo
havina maana kama mhusika anakosa sifa za ndani ambazo ndizo hasa
zinazomfanya mwanaume awe mume bora au baba bora.
Hujawahi kuona wanandoa ambao walioana kwa ndoa za kifahari, wakaishi maisha ya duniani kama wapo peponi kutokana na utajiri mkubwa walionao, mwisho wakaachana na kupeana talaka kwa vurugu kubwa?
Hujawahi kuona wanandoa ambao walioana kwa ndoa za kifahari, wakaishi maisha ya duniani kama wapo peponi kutokana na utajiri mkubwa walionao, mwisho wakaachana na kupeana talaka kwa vurugu kubwa?
Hujawahi kusikia wanawake ambao licha ya waume zao kuwa na kila kitu,
zikiwemo fedha nyingi, magari ya kifahari na majumba ya maana
wanazikimbia ndoa zao na kwenda kuolewa na walala hoi? Mifano hiyo
inatosha kukufanya ujiongeze kwamba kumbe ubora wa mume au mwanaume, ni
zaidi ya vile ambavyo watu wengi wanaamini.
Kwa kuwa mimi si mjuzi wa kila kitu, huwa napenda zaidi kusikia kutoka
kwako msomaji wangu. Hebu niambie, kama sifa hizo za nje siyo zinazoweza
kutoa tathmini ya ubora wa mume, kumbe mwanaume au mume bora anapaswa
kuwa na sifa na vigezo vipi? Nitumie ujumbe mfupi kwa namba za hapo juu
na wiki ijayo tutahitimisha mada yetu.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment