tiko
tiko
Askari
wanne wa jeshi la polisi Tanzania wamejeruhiwa kwa risasi baada ya
kutokea mapigano kati yao na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika
mapango ya Amboni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi la Polisi CP Paul Chagonja
Akitoa
taarifa rasmi ya jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo, Kamishna wa
Oparesheni na Mafunzo wa jeshi la Polisi CP Paul Chagonja aliyelazimika
kusafiri kwa helkpta kutoka Dar es salaam kwenda Tanga, amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa si tukio kubwa kama
linavyoelezwa na baadhi ya watu na kwamba waliohusika ni majambazi na
siyo magaidi.
Amesema
kilichotokea ni oparesheni ya kawaida iliyofanywa na jeshi la polisi
kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliodaiwa kujificha katika
mapango hayo na ndipo yalipotokea mapigano hayo yaliyoambatana na
kurushiana risasi na kupelekea askari hao kujeruhiwa.
Amesema
baada ya hali kuwa tete, jeshi hilo lililazimu kuomba msaada kutoka kwa
askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ambao walifika katika eneo la
tukio na kufanikiwa kutuliza hali ya taharuki iliyokuwa imetanda katika
eneo hilo.
Kamishna
Chagonja amesema askari waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo, na kwamba jeshi hilo
linaendelea na msako ambapo hadi sasa hakuna alikamatwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda ambao ni watu wanaoishi maeneo ya jirani na
mapigano hayo pamoja na mwanahabari wetu, wamesema kuwa mapigano hayo
yaliyoanza jana usiku na kuendelea hadi usiku kucha na kwamba mwanajeshi
mmoja wa JWTZ anahofiwa kuuawa na mwili wake umepelekwa katika
hospitali hiyo ya Bombo.
Alipoulizwa
kuhusiana na madai ya kuwepo kwa kifo cha mwanajeshi mmoja, CP Paul
Chagonja amesema kuwa Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa taarifa
inayohusu wanajeshi wa JWTZ, na kuwataka wanahabari waulizie suala hilo
kwa msemaji wa JWTZ.
Tumemtafuta
msemaji wa JWTZ Meja Joseph Masanja ambaye amesema kuwa si jukumu lake
kutoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo, kwa kuwa tukio hilo ni la
kipolisi na siyo la kijeshi.
“Ukitaka
kujua taarifa yoyote kuhusu tukio hilo waulize polisi, kwa kuwa hilo ni
tukio la kipolisi, sisi huku hatuna taarifa yoyote” amesema Meja
Masanja.
Mwanahabari
wetu alipotaka kupata taarifa zaidi kutoka katika hospitali ya Bombo
ameambiwa kuwa polisi imewazuia kutoa taarifa yoyote kuhusiana na suala
hilo.
Alipojaribu
kumuuliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Said Magalula kuhusu kifo cha
mwanajeshi mmoja, Mkuu huyo wa mkoa alikiri kupata taarifa za kifo hicho
bila kueleza zaidi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment