tiko
tiko
STAA wa
filamu nchini, Wastara Juma amesema anajihisi kupoteza mwelekeo
unaomfanya kushuka kisanaa tokea kufariki kwa mumewe, Juma Kilowoko
‘Sajuki’ kwani ari yake ya kufanya kazi imepotea.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi
karibuni, alisema Sajuki alikuwa ni msaada mkubwa sana kwake kisanaa
mbali na maisha ya kawaida, kwani anashindwa kupita njia alizokuwa
anapitishwa na mumewe huyo kiasi cha kujikuta akitoa filamu kati ya
mbili hadi tatu kwa mwaka.
“Nikiri tu kwamba nimeshuka kisanaa,
kasi ya kipindi kile imepungua, mume wangu alikuwa akijituma kuhakikisha
mikakati yetu inaenda, kwa mwaka mzima nilitoa filamu hata tatu lakini
toka asa naambulia moja tu mwaka mzima,” alisema.
tiko
tiko
Post a Comment