tiko
tiko
Moja
ya story zilizochukua headlines kutoka Uganda leo January 13, ni ile
inayohusu Waandishi wa habari nchini humo kuandamana baada ya Afisa wa
Polisi Joram Mwesije, kumpiga mwandishi Adrew Lwanga, na
baadae akakutana na Ispekta wa Polisi na kukiri makosa yake, pamoja na
kukubali kulipia gharama zote za matibabu za mwandishi huyo.
Waandishi hao waliandamana hadi makao
makuu ya Polisi na kutaka kukutana na mkuu wa Polisi kwa lengo la
kuhakikishiwa mazingira salama ya kufanya kazi, baada ya mwandishi
mwezao kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Afisa wa Polisi, Maandamano
yaliyoanza baada ya kikao walichoafikiana kutokuandika habari zozote
kuhusu shughuli za Polisi hadi Afisa aliyefanya tukio hilo akamatwe na
kuachishwa kazi.
“Likuwa
mbaya sana hiyo Journalist hiyo ni watu wa kusave hii nchi yetu sasa
kuona hiyo mambo ya kupiga Journalist tuliona hiyo kitu ni mbaya, sasa
tulisema tunataka tutembee tufike huko Naguru tuone IGP, tumuambie kila
kitu tumeona hapa Journalist tunataka kupigwa sasa watuache tufanye
kazi yetu.“- MWANDISHI
Mwandishi wa habari aliyepigwa na kujeruhuwa akiwa kazini amelazwa katika kumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Msambia, nchini humo.
Nimekurekodia taarifa hiyo kutoka kituo cha WBS Uganda…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga
na mimi
tiko
tiko
Post a Comment