tiko
tiko
Mastaa
wengi tumeona wakijichora tattoo sehemu mbalimbali za mwili, sikuwahi
kusikia kwamba kuna mtu amewahi kujichora tattoo kwenye jicho.
Story iko hivi, rappa mmoja toka Marekani, Mace
ameingia kwenye headline, story yake ni kama ya kushtua hivi, yeye
alijichora tattoo kwenye jicho lake la kushoto, sio kwenye ngozi kama
ambavyo tumezoea!
Msanii huyo alikimbizwa Hospitali baada
ya kupata maumivu makali ya jicho ambalo alichora tattoo, kwa bahati
nzuri alifanikiwa kupatiwa matibabu.
Tattoo hii ni tofauti na tattoo za
kwenye ngozi, hii ya kwenye jicho huchorwa kwa mtindo wa wino kuingizwa
ndani ya jicho na kisha kuenea ndani ya jicho kama wingu jeusi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment