tiko
tiko
UKATILI wa kijinsia unaendelea kutikisa katika mkoa wa Mara, ambapo mwanamke mmoja, Robhi Mwita, amelazwa katika Hospitali Teule ya wilaya ya Bunda, baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kuingiziwa chuma sehemu za siri na mume wake, aliyetajwa kuwa ni Mwita Chacha Chirare, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo lililoripotiwa katika Kituo
Kikuu cha Polisi Bunda lilitokea Januari 2, mwaka huu, majira ya saa
2:00 asubuhi katika kijiji cha Butakare, nje kidogo ya mji wa Bunda.
Kwa sasa, mwanamke huyo amelazwa katika
Hospitali ya Teule ya wilaya ya Bunda. Akisimulia mkasa huo akiwa
hospitalini, mwanamke huyo alisema siku hiyo mume wake aliyekuwa amelala
kwa mke mkubwa, alifika nyumbani hapo na kumkuta akiwa anakamua ng’ombe
maziwa.
Alisema; “Baada ya kufika nyumbani,
alimuuliza binti yetu niko wapi, alipoambiwa ninakamua ng’ombe
alinifuata zizini na kuanza kunigombeza kuwa usiku wa siku hiyo
niliingiza mwanamume ndani na kufanya naye tendo la ndoa.
Tukio hilo lililoripotiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Bunda lilitokea Januari 2, mwaka huu, majira ya saa 2:00 asubuhi katika kijiji cha Butakare, nje kidogo ya mji wa Bunda.
Kwa sasa, mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali ya Teule ya wilaya ya Bunda. Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini, mwanamke huyo alisema siku hiyo mume wake aliyekuwa amelala kwa mke mkubwa, alifika nyumbani hapo na kumkuta akiwa anakamua ng’ombe maziwa.
Alisema; “Baada ya kufika nyumbani, alimuuliza binti yetu niko wapi, alipoambiwa ninakamua ng’ombe alinifuata zizini na kuanza kunigombeza kuwa usiku wa siku hiyo niliingiza mwanamume ndani na kufanya naye tendo la ndoa.
“Nilijitetea sijafanya hivyo, lakini akaanza kunishambulia kwa kipigo na kuninyonga shingo kwa kutumia kitenge hadi nikaanguka na kupoteza fahamu.
Nilipozinduka nikajikuta mimi na binti yetu mwenye umri wa miaka 13 (jina linahifadhiwa) tumefungwa mikono, baadaye akatufungulia na kuanza kutupiga kabla ya kutokomea.
Alisema wasamaria ndio waliomsaidia kumfikisha Polisi na baadaye hospitalini anakoendelea na matibabu. Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Philipo Kalangi alisema tukio hilo bado halijaripotiwa kwake.
Alisema atafuatilia kwa Mkuu wa Polisi Bunda, ili aweze kutoa taarifa kwa vyombo vya habari. Muuguzi wa zamu katika wadi ya wanawake hospitalini hapo, Esther Maduhu, alisema mwanamke huyo alipokelewa akiwa na hali mbaya na kwamba kwa sasa hali yake inaendelea vizuri
tiko
tiko
Post a Comment