tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Bw. Richard Abdoni Juma, (44) anayedaiwa kupata ajali na kuvunjika nyonga.
Muumini wa Kanisa la Jehova Witness, Richard Abdoni Juma, 44, (pichani),
mkazi wa Mtaa wa Migera wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, ambaye
alitarajiwa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kutokana na ajali, madaktari wameshindwa kufanya hivyo kutokana na imani
ya dini yao.
AGUNDULIKA HANA DAMU
Akizungumza na waandishi
wa gazeti hili wiki iliyopita katika wodi namba 17, Sewahaji mgonjwa
huyo alisema kwamba madaktari waligundua kuwa amepungukiwa damu hivyo
walimuomba aongezewe kwanza ndipo wamfanyie upasuaji lakini alikataa.
“Nimekataa kuongezewa damu kutokana na imani ya dini yangu ya Jehova Witness ambayo inakataza mtu kuongezewa damu.
“Baada ya kuwaambia
madaktari hao hilo walinishauri nitumie vyakula vinavyoongeza damu
yakiwemo matunda na wakasema watanifanyia upasuaji baada ya damu
kuongezeka.
CHANZO CHA TATIZO
“Nakumbuka ilikuwa
Jumapili ya Desemba 28, mwaka jana saa 7 mchana maeneo ya Amgembe
Nyangoye wakati nikitoka kanisani kusali huku nikiwa nimempakia mwanangu
Lucas (11) kwenye pikipiki ndipo gari dogo ghafla lilikatisha barabara
tukaligonga wote tukaanguka na kuumia.
“Mwanangu Lucas aliumia
vidole na mguu, mimi nilihisi maumivu makali sana mwili mzima lakini
nyonga ndiyo ilikuwa ikiniuma zaidi, wasamaria wema walifika na
kutuchukua kisha kutukimbiza katika Hospitali ya Wilaya Bukoba.
“Hali ilizidi kuwa mbaya
kitendo kilichofanya madaktari wanihamishie katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, Mwanza baada ya wiki moja kupita, wakati huo mwanangu alibaki
hospitali ya Bukoba kisha akaruhusiwa kwenda nyumbani.
NILIGUNDULIKA NYONGA IMEVUNJIKA
“Nikiwa katika Hospitali
ya Bugando nilifanyiwa uchunguzi sambamba na vipimo ikagundulika kuwa
nyonga imevunjika hivyo nihamishiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Nilipewa matumaini
kwamba katika hospitali hiyo kuna madaktari bingwa na ilipofika Jumanne
ya wiki hii (wiki iliyopita) nikahamishiwa hapa.
Richard Abdoni Juma akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
MADAKTARI WATAKA KUMPASUA
“Mbali na kugundulika
kuwa nyonga ilivunjika lakini ilibainika kuwa nina upungufu wa damu
hivyo natakiwa kuongezewa damu kwanza ndipo nifanyiwe upasuaji, hata
hivyo, kutokana na imani ya dini yetu nilikataa.
“Imani yetu haturuhusiwi kuongezewa damu hivyo madaktari nilipowaambia hivyo wakaahirisha zoezi hilo.
“Badala yake walinishauri
nitumie matunda mbalimbali kwa imani kuwa ndani ya wiki moja damu
itakuwa imeongezeka ndipo watakaponifanyia upasuaji.
NATUMIA MATUNDA YA KUONGEZA DAMU
“Kutokana na ushauri huo
sasa natumia matunda ya kuongeza damu kwa wingi hivyo naamini baada ya
muda huo walionishauri nitakuwa nimeimarika.
KAZI YAKE
“Mimi ni fundi ujenzi na
nina mke na watoto watatu ambao wananitegemea lakini kwa sasa wamekosa
matumaini ya kuishi kutokana na kuwepo kwangu kitandani, sijiwezi,
kuinuka nimekuwa ni mtu wa kujisaidia hapahapa nilipo, ni mtu wa
kuogeshwa.
“Ninawashukuru madaktari
na manesi wa hapa Muhimbili kwa kunipa huduma za karibu, nawaombeni
Watanzania mnisaidie kwa kupitia namba yangu 0784 969568 au 0763
196457,” alisema Richard akiwa amejilaza kitandani.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment