tiko
tiko
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.
Wakati
Jeshi la Polisi likiwa kwenye operesheni ya kuwasaka watu wanaovamia,
kuteka vituo vya polisi na kupora silaha, Mbunge wa Arusha Mjini
(Chadema), Godbless Lema, amemgeukia Kamishna wa Operesheni na Mafunzo
wa Jeshi hilo, Paul Chagonja, akisema anahusika katika kupanga mkakati
wa kutekeleza vitendo hivyo vya uhalifu.
Amesema
mkakati huo umepangwa na Kamishna Chagonja kwa nia mbaya ya kumhujumu
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, ili
kuchafua taswira ya uongozi wake mbele ya macho ya jamii.
Lema
alisema hayo wakati akichangia mjadala kuhusu taarifa ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa na
Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe, bungeni juzi.
Alisema
kutokana na nchi kufikia kuwa mithili ya 'gheto', ambamo kila anayeishi
humo ana uhuru wa kufanya anavyotaka, katika Jeshi la Polisi, Chagonja
haamini kama Rais Jakaya Kikwete amekwishafanya uteuzi wa IGP na hivyo,
kujiamulia kufanya mambo anavyotaka.
Lema
alisema hali hiyo ni uthibitisho dhahiri wa taarifa alizonazo kwamba,
jeshi hilo limepasuka vipande viwili, ambavyo kila upande unafanya
unavyotaka.
"Na
mimi nikiwaambia na nimelichunguza. Jeshi la Polisi limepasuka. Ma-RPC
(makamanda wa polisi wa mkoa) wanalalamika. Chagonja haamini kama Rais
ameshafanya uteuzi wa IGP," alisema Lema.
Aliongeza: "Na mimi nasema hata hizi bunduki zinaoibwa inaweza ikawa mkakati wa Chagonja ku-subotege (kumhujumu) IGP."
Alisema
hata Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, pamoja na watu
wote duniani wanaujua mkakati huo wa Chagonja, lakini wote wanashindwa
kupaza sauti kuueleza.
"Hii
nchi ni kama gheto, yaani nchi ni kama gheto kabisa. Hujui serikali iko
wapi. Na tukiongea humu kuwashawishi wananchi wawe imara tunasemwa
tunachochea vurugu," alisema Lema.
tiko
tiko
Post a Comment