tiko
tiko
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya bunge ya hesabu za serikali Ferister Bura
Wametaka
hatua hiyo ichukuliwe dhidi yake kutokana na uzembe alioufanya katika
ofisi yake uliosababisha wakuu wa idara zote za halmashauri hiyo kukaimu
nafasi zao kwa muda mrefu sasa.
Pia
halmashauri hiyo imeagizwa kushirikiana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuhakikisha inajibu maagizo manne na
hoja 21 za ukaguzi haraka iwezekanavyo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Felister Bura ambaye pia
aliongeza kuwa ofisa huyo amekuwa sababu ya idadi kubwa ya watumishi wa
halmashauri hiyo kutopandishwa vyeo na kuwa na wakuu wengi wa idara
wanaokaimu.
“Wakuu
wengi wa idara katika halmashauri hii wanakaimu wengine zaidi ya miaka
sita na nane tena wenye sifa stahiki hii ni dhambi; ashushwe cheo ili
naye aone maumivu yake huu ni uzembe wa hali ya juu hatuwezi
kuuvumilia,“ alisisitiza.
Kaimu
mwanasheria wa halmashauri hiyo, Gabriel Lunyamila aliwaeleza wajumbe
wa kamati hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu amekuwa akikaimu nafasi hiyo
licha ya kuwa na sifa stahiki.
“Nilianza
kama Ofisa kata 1993 na baadae nikajiendeleza na kuwa mwanasheria
katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kisha mwezi Machi 2011
nikahamishiwa katika halmashauri hii ya Nkasi hadi kufikia Oktoba mwaka
jana nadai zaidi ya Sh milioni moja ikiwa stahiki zangu za kukaimu
nafasi hii ambazo bado sijalipwa,“ alieleza.
Kwa
upande wake, Ofisa Usimamizi Fedha wa Tamisemi na Mratibu wa Kamati za
Hesabu za Serikali za Mitaa Wizarani, Fauzia Hamidu alikiri kuwa tatizo
kubwa katika halmashauri ya Nkasi ni kutopandishwa vyeo kwa watumishi
wake na pia idadi kubwa ya wakuu wa idara wanakaimu.
Alisema tatizo lipo kwa Ofisa Utumishi ambaye amechelewesha kuwasilisha mchakato wa kupeleka katika vikao husika kufanyiwa kazi.
tiko
tiko
Post a Comment