tiko
tiko
Familia
ya watu 18 wakiwemo watoto 10 wa kata ya mwembesongo manispaa ya
morogoro wameendelea kulala nje kwa siku 23 sasa huku wakinyeshewa mvua
kufuatia kufukuzwa kwa nguvu kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi na
kuiomba serikali iwasaidie.
Paparazi
imefika katika eneo hilo na kukuta watu hao wengiwao ni watoto wakiwa
bado wanaendelea kuteseka na hali ngumu wanayoipata kulala nje na
kunyeshewa mvua ambapo wakiongea kwa uchungu huku wakionyesha hati
halali ya umiliki wa nyumba yao wameiomba serikali kuwasaidia.
Baba
mzazi wa familia ambaye anadaiwa kuuza nyumba hiyo Fredinandi
Kainyingi amesema watoto wake ndiyo wamiliki halali wa nyumba hiyo licha
ya kutoa ushahidi wa kutosha juu ya umiliki wa nyumba lakini vyombo
vinavyohusika bado vinawanyima haki na kushindwa kujua nini hasa lengo
la vyombo hivyo.
Naye
mwenyekiti wa mtaa wa Jumahamsini Omari Makiluka na majirani wamesema
wanajitahidi kuwapa misaada ya chakula ingawa hawanauwezo wa kuwapa
huduma ya ladhi watu wote hao na wameimba serikali na mashirika ya
haki za binadamu kuingilia kati kuona uwezekano wa kuwasaidia.
tiko
tiko
Post a Comment