tiko
tiko
Mkurungezi wa Bendi ya African Stars
‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka amemuonya msanii anayefanya vizuri kwenye
muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutojaribu kujihusisha na
utumiaji wa madawa ya kulevya na kusema akijaribu atapotea.
Akizungumza na Ijumaa hivi karubini,
Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema Diamond anaweza kufanya vizuri kwa miaka
mingi inayokuja lakini akijaribu kutumia dawa hizo ataishia pabaya.
“Tumeona wasanii wengi wa Tanzania ambao
awali walikuwa wanafanya vizuri lakini baada ya kujaa sifa na kukutana
na marafiki wengi pamoja na makundi wakazama kwenye dawa za kulevya na
sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu wakati wenyewe wamejiharibia,”
alisema Iron Lady.
Wasani ambao awali walikuwa wakifanya
vizuri kimuziki lakini baadaye ‘wakadrop’ baada ya kujiingiza kwenye
matumizi ya unga ni pamoja na Chid Benzi, Ray C, Q Chiller, Lord Eyez,
Msafiri Diof na wengine ambao sasa wameshafariki.
tiko
tiko
Post a Comment