tiko
tiko
Mwaka
2014 umeanza kwa Wasanii kadhaa wa bongofleva wakiwemo wa zamani na wa
sasa kuonyesha mali zao kama magari pamoja na nyumba wanazomiliki au
wanazozijenga.Post ya leo inamuhusu Jux ambae siku kadhaa zilizopita alikua kwenye headlines za millardayo.com kuhusu video yake ya ‘uzuri wako’ aliyoifanya China kufungiwa kuonyeshwa kwenye vituo vya TV.
Jux kwenye Exclusive interview na millardayo.com anasema hawezi kutaja kiwango cha pesa alichokitumia kulinunua hili gari ila ni pesa ambayo imetokana na biashara anazozifanya.
Ukiangalia bei nyingi za hii Nissan FUGA kwenye mtandao, nyingi zinaanzia dola elfu mbili na zinafikia mpaka dola elfu 4 ambayo ni zaidi ya milioni sita za Kitanzania, hapo bado kusafirisha, kulipa ushuru na mambo mengine muhimu.
tiko
tiko
Post a Comment