Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

UKIONA RAFIKI YAKO AMEPOST UJUMBE KAMA HUU BASI JUA KWAMBA WABAYA WAMESHAINGIA KWENYE AKAUNTI YAKE

tiko tiko
http://www.secureidnews.com/wp-content/uploads/2014/08/Hackers-With-An-Agenda.jpg
Sina shaka kwamba pengine ni wewe au mmoja wa marafiki zako umewahi kuona amepost ujumbe kama huu hapa chini na pengine kwa kutojua ukamlaumu. Hawa ni watu wanaotumia udhaifu wa wengine kutoajua jinsi ya kulinda akaunt zao kwa kuingia kwenye akaunti zao na kutangaza kile walichodhamilia katika akaunti  hiyo. Tafadhari usijaribu kufuata huyo ujumbe wala kujisajili kwa kuweka e-mail yako katika mtandao huo. Kama ni rafiki yako wa karibu ni vyema ukamjulisha pengine kwa simu kwamba abadilishe password katika akaunt yake. Maelekezo haya nimarefu kuyajua kwa ukamilifu, endelea kufuatana nasi kujua zaidi ili uweze kuwa salama.



WANAWEZAJE KUINGIA KWENYE AKAUNTI YA MTU?
Kuna njia nyingi zinazotumika kuingia katika akaunti ya mtu. Nyingine zinasababishwa na uzembe wa watumiaji wa mitandao kwa kutojua maana au nini cha kufanya kuweka akaunti zao salama. Kwa sasa nisingependa kueleza njia zinazotumika kwa kuamini kwamba nitachochea zaidi na kuongeza idadi ya watu wanaingia kwenye akaunti za wengine, jambo ambalo si zuri. Bali nitajikita katika kueleza ni jinsi ganiunaweza kuzuia akaunti yako isiingiliwe kirahisi au uweze kujua mara moja kwamba kuna mtu anajaribu kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook au e-mail. Wakati mwingine ni Uzembe unaofanywa na watumiaji wa Facebook, Bonyeza Hapa kujua juu ya uzembe unaofanywa na watumiaji wa Facebook unaosababishwa waingiliwe kwenye akaunti zao. Matapeli waliopo sasa wanapost ujumbe huu happa chini wenye rangi nyekundu, ikiwa ni njia ya kuwafikia watu wengi na kufanya utapeli.

"NAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS. Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo TANZANIA -LOAN ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA. Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusiana ma jaws TANZANIA-LOAN pia sikua na uhakika nayo. Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji. Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http tanzania-Loan.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs.125,000 ( LAKI NA ISHIRINI) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure! Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani LAKI 125 ni kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia LAKI 125 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 6,000,000 (Million 6) hapo nilipo siamini friends. ‪#‎USHAURI‬: Nifungue mradi gani nina hizi Million sita, kwani nilikua sijajipanga nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu. Pia kwa yoyote ambae atahitaji kutembelea tovuti ya hawa jamaa wa mikopo, bonyeza hapa: http://tanzania-Loan.wapka.mobi"


Ujumbe huu hapo juu ni ujumbe wa matapeli na hauna ukweli wowote na umekuwa ukizagaa kwenye mtandao wa Facebook kupitia akaunti za watu tofauti amabazo zimeshaingiliwa. Ukiona ujumbe huu umekuwa posted na rafiki yako amini kwamba si yeye kapost bali kaingiliwa na watu. Bonyeza hapa kusoma makala ya kwanza jinsi ya kuzuia wasiingie kwenye akaunti yako.

TUNGEPENDA UTOE MAONI YAKO HAPA CHINI NA KAMA UNGEPENDA KUPATA MSAADA KUWEKA SALAMA AKAUNTI YAKO TOA MAONI YAKO KWA COMMENT HAPA CHINI WAHUDUMU WETU WATAWASILIANA NAWE KATIKA INBOX YAKO.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top