tiko
tiko
Taarifa zilizotoka muda mfupi uliopita kuhusiana na zoezi la utafutaji wa ndege iliyopotea ya AirAsia QZ 8501
zinasema kuwa vikosi vinavyohusika na utafutaji wa ndege hiyo vinasema
kuna uwezekano mkubwa imezama kwenye kina kirefu cha bahari.
Chanzo cha habari
kutoka nchini humo kinasema uchunguzi kuhusu ndege hiyo bado unaendelea
huku wakitumia ndege za kijeshi kutoka Indonesia na Singapore Kusini
Magharibi mwa Pwani ya Borneo ambapo ilipoteza mawasiliano.
Bado jitihada za kuwatafuta abiria 162
waliokuwepo ndani ya ndege zinaendelea,na mpaka sasa hakuna mawasiliano
yoyote,ilikua ikielekea Singapore.
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa
Surubaya nchini Indonesia na shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye
kisiwa cha Belitung.Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment