tiko
tiko
Upendo wa mama kwa mtoto wake hauwezi
kufananishwa na kitu chochote hapa duniani,kwa hili nadhani hakuna
anaebisha.Ila ni ukweli pia wazazi hutofautiana katika kuonyesha mapezi
kwa watoto wao,hapa nazungumzia mahusiano ya wazazi na watoto katika
maisha ya kila siku.
Kwa sisi watoto wa maika ya 1980+ wazazi
wetu wengi walitufanya tuwaogope na kuwaheshimu hata kwanidhamu ya
woga, kitu ambacho mimi nakipinga sana.Leo mambo ni tofauti sana, wazazi
wengi wamekuwa wakijitahidi kujenga urafiki na watoto wao na hivyo
kuleta ukaribu na uwazi baina yao, kitu ambacho ni kizuri zaidi kwa
ulimwegu huu wa sayansi na tekelinalokuijia.
Turudi kenye mada
Kama umekuwa ni mtu kumfuatilia
mwigizaji Kajala Masanja, naamini utakubaliana na mimi kuwa Kajala na
binti yake Paula, bali ya kuwa na mahusiano ya mtu na mtoto wake lakini
wanaishi kama mtu na rafiki yake.
Hiki kitu huwa kinanikosha sana, kwani
naamini hii uongeza ukaribu na upendo baina yao,pia inatoa fursa ya
mtoto kuwa muwazi kwa mzazi wake. Mara zote wamekuwa wakionekana kuwa
pamoja kwenye hali zote, furaha nahata udhuni.Naamini katika malezi ya
namnahii hutoa nafasi kwa mzazi na mtoto kuzungumza kwa uwazi na
kushauriana katika jambo lolote.
Hongera sana Kajala kwa kutuonyesha
hili,naamini wengi watajifunza kupitia wewe, kwangu wewe ni mama na
mlezi bora zaidi kwa mwaka huu.
Jionee baadi ya picha za Kajala akiwa na mtoto wake Paula.
tiko
tiko
Post a Comment