Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Picha 12 za gari alilonunua msanii Shetta na mambo matatu aliyoyasema kwa wanaotaka kufanikiwa.

tiko tiko
s9Lengo lilikua ni kukutana na Shetta kwa ajili ya kufanya interview kuhusu Tour yake ya Kerewa aliyotembea nayo kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania kwenye maeneo mbalimbali kama Mombasa Kenya, so ilikua iwe hivyo lakini kwa bahati nzuri akawa amekuja na hili gari nikalazimika kumuomba tupate za ndani kidogo itupe nguvu ya kuzichanga.
Shetta ni staa wa single kama ‘Nidanganye‘ na ‘kerewa‘ ambazo zote alimshirikisha staa mwingine wa bongofleva Diamond Platnumz ambapo kwenye hii post ya leo on millardayo.com ameziachia exclusive kadhaa za hatua zake za kimaisha.
Anasema kwa yeyote ambae anahitaji mafanikio kwenye hii dunia ni lazima awe na Uvumilivu, uelewa wa kwamba sio kila siku utapata, matumizi mazuri ya kinachopatikana hata kama ni kidogo, kujifunza kuweka akiba, kuishi na watu vizuri bila kujali unamjua au haumjui pamoja na bidii kwenye kila nafasi ndogo unayoipata, hayo ni baadhi ya mambo ambayo anasema yanaweza kukuweka karibu na mafaniko au kukupa mafaniko.
s11Gari hili ambalo ni aina ya Harrier Lexus ni la tatu toka Shetta aanze kumiliki magari ambapo gharama yake ni shilingi milioni 45 kwenye sehemu mbalimbali za kuuzia magari Tanzania…… kama unataka kujua zaidi kuhusu Shetta itabidi ujiunge na mimi kwenye AMPLIFAYA ya CloudsFM saa moja usiku.
s12Mara nyingi huwa wengi wakiona picha kama hizi wanauliza una nyumba? goodnews ni kwamba kwa sasa Shetta anamalizia kujenga nyumba yake Madale Dar es salaam hivyo ameahidi kushare pichaz na sisi sio kuringishia bali kutoa hamasa kwa vijana wengine wanaomchukulia kama mfano kujifunza na kupata nguvu ya kupambana kuzichanga kutoka kwenye hali ya chini kama yeye alieanzia muziki akiwa shule ya sekondari Jitegemee.
s13
s8
s7
s6
s5
s4
s3
s2
s1Unataka stori kama hizi zisikupite? unataka kuwa kupata kila kinachonifikia? karibu ujiunge na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top