tiko
tiko
Pamoja
na kutoendelea kuzungumziwa sana katika vyombo vya Habari,lakini
Mataifa mengi yameendelea kuathiriwa na ugonjwa Ebola ambao bado
umeendelea kuwa tishio.Nesi ambaye alikua akitoa msaada kwa wagonjwa hao nchini Sierra Leone juzi jumapili usiku amegundulika kuambukizwa ugonjwa wa Ebola mara baada ya kurejea kwao Uingereza.
Kwa sasa anatabiwa katika hospitali ya Rartnavel jiji la Glasgow kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Afya la UK, Jeremy Hunt ambaye alithibitisha habari hizo.
Katika taarifa iliyotolewa na Shirika la utangazaji la BBC uchunguzi uliofanyika umethibitisha ni kweli mkunga huyo ameambukizwa ugonjwa huo na tayari ametengewa chumba chake maalum kabla ya kuhamishiwa hospitali nyingine iliyopo Kaskazini mwa London haraka iwezekanavyo.
Hospitali anayokwenda kutibiwa ndio ambayo mkunga mwingine kutoka Ujerumani Willium Pooley alilazwa hapo baada ya kubainika kuumwa.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment