tiko
tiko
Kijana
mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, leo usiku
amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati akiingia Club
Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam.
Tukio
hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku ambapo kijana huyu akiwa na
rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliokuja
nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa
risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana.
Shuhuda
wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo
nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi
sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa
imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo.
shuhuda
huyo aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia
"pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi
za watu hao waliokuwa wamevamiwa.
Waliotenda
tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio baada ya watu kujaa eneo
ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa ameanguka chini.
Polisi
walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu
nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa
amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana
ilikuwa ikitoka nyingi sana, walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha
katika hospitali ya jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia
njiani akikimbizwa kuelekea hospitali
Tukio
hili linaonekana nila kulipiza kisasi ingawa taarifa kamili bado
hazijajulina, endelea kufatilia blog yetu kujua mwendelezo wa tukio hili
la kusikitisha
tiko
tiko
Post a Comment