tiko
tiko
KATIBU
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda
Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili
kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu
Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka
aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na
Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi
Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu
wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002
(kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya
Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu
Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C.
Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia
imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana,
Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na
Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza
tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu
zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa
Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza
kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme
(TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha
tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali
lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya
Kimataifa (ICSID).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014
tiko
tiko
Post a Comment