tiko
tiko
Kama
ulifanikiwa kuisherehekea Christmas ya mwaka huu 2014 kwa amani basi ni
heri kwako, kumbe wakati wengine wakisherekea kwa amani Sikukuu hii
kubwa ya mwaka kuna sehemu ambazo hakukuwa na heri yoyote siku hiyo.
Story hii ya kusikitisha inatoka Kenya ambapo jamaa mmoja Daniel Imonje,
alimpiga mke wake kwa shoka mpaka kufariki, majirani walioshuhudia
wakisema eti kisa ilikuwa ni kitendo cha mke wake huyo kutomuandalia
mume wake nyama ya kuku siku ya Christmas, badala yake akaandaa rosti ya
nyama ya ng’ombe.
Ni wengi waliolaani kitendo hicho
kilichotokea Kijiji cha Shanderema, Kenya na mashuhuda wamesema Daniel
alifanya unyama huo akiwa amelewa.
Mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kakamega baada ya kufanya mauaji hayo kwa ajili ya uchunguzi.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment