tiko
tiko
MTOTO wa
miaka sita, Bernard Benjamin ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya
Msingi Nyamunge, wilayani Ilemela jijini Mwanza, amesombwa na mafuriko
na mwili wake kukaa siku kumi na tano bila kuharibika.
Tukio hilo lilijiri Desemba 2, mwaka huu
kwenye Mto Kenge jijini hapa, maeneo ya Mabatini, Wilaya ya Nyamagana
baada ya kujaa maji ambapo marehemu alisombwa na mafuriko hadi pembezoni
mwa Ziwa Victoria.
Baba mzazi wa marehemu Bernard, Benjamin
David alisema siku ya tukio yeye alikuwa safari na mama wa mtoto
alikuwa kazini, watoto walibaki na msichana wa kazi nyumbani.
“Ilikuwa Jumanne asubuhi, mvua kubwa
sana ilinyesha kwa saa moja na nusu hivi na kusababisha mafuriko. Watoto
wangu wote walikuwa nyumbani, lakini mvua ilipokatika walitoka nje na
kuanza kucheza.
“Marehemu alikuwa anaondoka bila kuaga
kama mara tatu na kila alipofuatwa alikutwa akicheza pembezoni mwa mto
huo ambao umepita jirani na nyumba yangu.“Katika hali ya kushangaza
mara ya tatu wenzake walimfuata na kuanza kurudi naye wakati huo
marehemu alikuwa yupo nyuma ndipo aliteleza na kutumbukia kwenye maji ya
mto.
Mwili wa marehemu Bernard Benjamin ukiwekwa kaburini.
“Alipiga kelele na wenzake walivyosikia
sauti nao walipiga mayowe, mmoja wao alijitosa kwenye maji ili amuokoe
lakini kasi ya maji ilimshinda na kujikuta akijiokoa mwenyewe kwa
kushika mti, watu wakamuwahi na kumuokoa.
“Tuliutafuta mwili tangu siku hiyo hadi
Jumatano ya Desemba 17. Saa 10 jioni mke wangu alipigiwa simu na mtu
aliyejitambulisha kuwa ni muumini wa kanisa kwetu, akasema kuna mwili wa
mtoto umekutwa ufukweni mwa Ziwa Victoria eneo la Miti Mirefu.
Mama mzazi wa marehemu Bernard Benjamin akiweka mchanga kaburini.
“Nilikwenda na kukuta polisi
wameshafika. Nilipouona mwili niliutambua kuwa ni wa mwanangu akiwa
ameshafariki dunia lakini haukuwa umeharibika.“Bado alikuwa na nguo
alizovaa siku ya tukio, viungo vyake vyote vilikuwa salama ila mwili
ulikuwa mweupe sana kutokana na kukaa muda mrefu kwenye maji.
Mtoto Bernard Benjamin enzi za uhai wake.
“Tuliupeleka mwili Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, madaktari walimfanyia uchungzi na kusema mwili haukuharibika
kutokana na kufukiwa na mchanga mwingi kwenye maji, nilimshukuru Mungu
kwa hilo,” alisema baba wa marehemu.Mazishi ya mtoto huyo yalifanyika
Alhamisi ya Desemba 18, mwaka huu katika Makaburi ya Nyakato Sokoni
jijini Mwanza.
tiko
tiko
Post a Comment