tiko
tiko
Nick Cannon na mkewe Mariah Carey ni miongoni mwa mastaa waliamua kutengana kwa mwaka huu huku kila mtu akionekana kuendelea na mambo yake.Licha ya kutengana kwao kuna uvumi kuwa wapo katika kutoelewana,huku Nick Cannon akisema hana sababu ya kutumia mashairi ya albamu yake mpya atakayoitoa wakati wowote kumfikishia ujumbe mke wake huyo kutokana na tofauti zao.
Cannon aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hajarekodi wimbo wowote wenye lengo la kumchafua Carey “Sitasema kitu chochote kibaya kuhusu Mariah Carey,sisi ni familia iliyotokea kwenye mizizi ya upendo’
Cannon mwenye miaka 34 na Mariah Carey mwenye miaka 45 walifunga ndoa yao April 2008 na kufanikiwa kupata watoto wawili lakini baadaye mwaka huu walitengana huku Cannon akiendelea kutoonyesha kumbagua kitu kinachodaiwa ndiyo chanzo cha kutengana kwao.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment