tiko
tiko
Jina lake ni Emmanuel Msuya ambae usiku wa November 30 2013 Escape
One Mikocheni Dar es salaam alitangazwa mshindi wa BSS kwa mwaka 2013 na
kuzichukua MILIONI 50 kutokana na matokeo kamili ya mizani hiyo ya
vipaji vya muziki kwa wachanga.Unaambiwa kabla ya hapo, Msuya hakuwahi kushika au kumiliki zaidi ya shilingi laki tano… yani aliwahi kupata shilingi laki tano mara moja tu siku alipolipwa pesa ya miezi mitatu iliyotokana na mkataba wa kuifundisha na kuisimamia Kwaya ya KKKT kucheza ili ikafanye video.
Mambo matatu makubwa aliyoyafanya kwa hizi milioni 50 za ushindi wa BSS…. >>> Msuya amenunua nyumba ya milioni 17 nyumbani kwao Musoma mjini kama unavyoiona hapa chini kwenye picha, amenunua hili gari lenye thamani ya milioni 9, amejenga studio hiyo hapo juu kwenye picha ambayo imegharimu milioni 12 na tayari ameshapata nyumba ya kufanyia biashara ya Stationary Musoma Mjini.
tiko
tiko
Post a Comment