Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba,Posta jijini Dar.
Akizungumza
na Paparazi alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa
akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na
kumuovateki na kuligonga gari lake. Aidha alisema kuwa alisikia maumivu
na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha
kwa ndani.
‘’Nashukuru
Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote
kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani,’alisema
Keisha.
TUPE MAONI YAKOTUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE!!!.
Post a Comment