tiko
tiko
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameubeza muungano wa vyama vya upinzani, maarufu kama Ukawa na kusema muungano huo utabadilika jina ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na kuitwa Ukiwa, baada ya Chama Cha Mapinduzi kutangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Urais.
Kinana
alisema mabadiliko hayo ya jina, yanatokana na kelele nyingi pamoja na
mikakati mingi wanayoizungumza ya kuchukua madaraka ya Urais, jambo
ambalo alilisema ni sawa na ndoto ya Abunuasi.
Alisema
siku zote mtu yeyote au chama chochote kilicho na mikakati, hakielezi
mikakati yake hadharani, kama wanavyofanya viongozi hao wa Ukawa katika
majukwaa mbalimbali wanayozungumza.
Alisema
mbali na hayo, vyama hivyo vya upinzani bado havijaaminiwa vya kutosha
na wananchi katika kuongoza nchi, hali ambayo bado inawapa wakati mgumu
zaidi kwa kuwa watanzania wengi wameendelea kukiamini chama cha
mapinduzi.
tiko
tiko
Post a Comment