tiko
tiko
Dua! Mwamitindo na mtangazaji ‘the big
name’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ametembelea kituo cha watoto
yatima kilichopo maeneo ya Ubungo jijini Dar kisha kuangushiwa dua ya
nguvu na watoto wa madrasa.
Wikiendi iliyopita Jokate alifika
kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali huku akiwa amejitanda kichwa chake
ambapo alijumuika na watoto hao naye akakaa kwenye mkeka ndipo
akazungukwa na watoto hao yatima kisha kuombewa dua ili abarikiwe na
mambo yake yaende vizuri.
“Nilifurahi kuombewa dua na watoto. Hata
hivyo, mimi sioni kama kuna tatizo, kikubwa zaidi Mungu tunayemuabudu
ni mmoja ambaye anamsikiliza kila mtu kwa hiyo hakuna shida mimi
kuombewa Kiislam,” alisema Jokate ambaye wikiendi iliyopita ilikuwa ni
‘bethidei’ yake huku akizindua ngoma yake mpya ya Leo Leo
tiko
tiko
Post a Comment