tiko
tiko
Kweli
mafahari wikigombana nyasi ndio uumia! Picha za mwanamziki Diamond
akiwa na mpenzi wake Zari wakiwa ndani ya gari alizoziweka mtandao
usiku wa kuamkia leo siku ya wapendanao na kuandika kwa maneno ya lugha
ya kingreza kuwa wanaelekea siku ya Valentine “Road to Valentine...”
Zilizua timbwili la maneno miongoni mwa mashabiki wa Diamond ambao
walikuwa wakisifia “Project hii” na wale wa Wema aka TeamWema walikuwa
wakiponda na kumshabulia sana mwanadada Zari ikiwemo kumuiga mtindo wa
nywele Wema. Hii ilipelekea watu kutupiana maneno makali na mazito
yanayoweza kukufanya msomaji upofuke macho.
Baada ya mvutano mrefu kuhusu picha hizo za Diamondi na Zari, Ikatupiwa
picha hiyo ya Wema akiwa na Ommy, hapo tena moto ukawaka wale wa
mashabiki wa Diamond wakaanza kuponda huku TeamWema wakisifia. Mwisho wa
siku watu wakaamua kuzileta pamoja ili watu waseme bila ushabiki kuwa
ipi ni project ya ukweli na ipi feki….
Nami nikaona nizilete hapa kwenu,ila sio kushindanisha bali upate
kuziona na kukupa ubuyu wa kile kinachoendelea kuhusina na picha za
mafahari hawa wawili wenye mashabiki wengi zaidi hapa Bongo.
Jamani mashabiki acheni kutukanana huko mitandaoni, mbona wenyewe hatukanani?
Mzee wa Ubuyu
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment