tiko
tiko
Neema imeendelea kubaki upande wa mshambuliaji Christiano Ronaldo
baada ya juzi kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na
kumfanya kuwa mfungaji wa tatu kwa kuwa na magoli mengi katika historia
ya soka la Hispania.
Katika mchezo wa juzi jumapili Ronaldo
alihitimisha ushindi wao kwa kufunga goli la pili na kumfanya kufikisha
jumla ya magoli 290.
Ronaldo ambaye pia mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or
ya mwanamichezo bora wa dunia kwa mara ya tatu ameshika nafasi hiyo
akiwa amecheza michezo 289 huku nafasi ya pili ikishikwa na Alfredo Di Stefano ambaye amecheza michezo 392 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Raul Gonzalez mwenye idadi ya magoli 323 katika michezo 741.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment