tiko
tiko
MWALIMU wa Shule ya Msingi Manga katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Mary Majilanga amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Utemini, mjini Singida kujibu shitaka la kukamatwa ugoni .
Katika
kesi hiyo ya madai namba 8 ya mwaka huu, mshitakiwa Mary anatakiwa
kulipa Sh milioni 8 za ugoni kwa kuishi kama mume na mke na mwalimu
mstaafu, Julius Magandi ambaye imeelezwa ni mume wa Severina Michael
Kisunga waliojaliwa kuwa na watoto watano tangu ndoa yao mwaka 1985.
Licha
ya kufunguliwa kwa kesi hiyo ya madai Januari 26 mwaka huu na kutolewa
hati ya kuitwa shaurini mara mbili, mshitakiwa amekuwa hahudhurii
mahakamani badala yake Magandi amekuwa akipeleka taarifa mahakamani kuwa
mshitakiwa ni mgonjwa.
Hata
hivyo juzi wakati kesi hiyo ikitajwa mbele ya Hakimu Fedinand Njau,
baada ya Magandi kusimama tena mahakamani na kudai mshitakiwa yupo
hospitalini anatibiwa, Hakimu Njau alimpa Magandi dakika tano
kuhakikisha anamleta mshitakiwa mahakamani.
Baada
ya nusu saa kupita hatimaye Magandi aliwasili mahakamani hapo akiwa
ameongozana na mshitakiwa na alipopandishwa kizimbani mshitakiwa alidai
kuwa alikuwa hospitali ya mkoa kutibiwa macho.
Akijibu
shitaka la kukamatwa ugoni, mshitakiwa Mary alidai kuwa mwanaume Julius
Magandi anayedaiwa kukamatwa naye ugoni ni mume wake halali na kwamba
wamefunga naye ndoa ya kimila tangu 2013.
Naye
Magandi alidai kuwa Mary ni mke wake wa pili aliyefunga ndoa ya kimila
baada ya kuasi Ukristo na kuamua kuibadili ndoa yake ya kanisani ya mke
mmoja kuwa ya wake wengi.
Kutokana
na Hakimu mwenye jalada la kesi hiyo kuwa safarini Dodoma kikazi,
Hakimu Njau aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 mwaka huu itakapoanza
kusikilizwa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment