tiko
tiko
MABINTI 22 wa
Kihindi na Kinepal walioingizwa nchini kufanya biashara ya kuuza miili,
wamenaswa wakimwaga machozi hadharani kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere, jijini Dar wakisikitikia kuwakosa wateja wao Wabongo ambao
inadaiwa walikuwa wakiwalipa vizuri.
Makahaba hao wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kurudi India.
Mabinti hao waliingizwa nchini kati ya Mei na Desemba, mwaka jana na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dhamaka Entertainment Center Limited, Omprakash
Singh kwa lengo la kuwafanyisha biashara ya ngono katika klabu
anazozimiliki.
Singh anadaiwa kuwa, alipowafikisha nchini makahaba hao, aliwapokonya
hati zao za kusafiria kisha kuwafanyisha kazi hiyo pasipo kuwalipa
mshahara ndipo Idara ya Uhamiaji nchini iliposimamia sakata hilo kwa
kumshtaki mkurugenzi huyo mahakamani ambapo mahakama iliamuru makahaba
hao walipwe mishahara yao na kurudishwa makwao.
Mapema wiki hii, chanzo makini kilimwaga ubuyu kuwa makahaba hao
wanarejeshwa makwao, bila kuchelewa, mapaparazi wetu walitia timu katika
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na kushuhudia makahaba hao
wakifikishwa na gari la Uhamiaji lenye namba za usajili STK 9632.
...Wakiwa na mizigo yao.
Baada ya kushuka, makahaba hao wakiwa katika sura ya huzuni, walisikika
wakilia huku wakidai wanarudishwa nchini kwao ambako hawakuwa na kipato
kikubwa kama walichokuwa wakipata Bongo.
“Kwa nini jamani wasituache wakati Bongo tumepazoea, tumetengeneza fedha nyingi wangetuacha tu kwanza tumeingia kihalali,” alisikika mmoja wa makahaba hao aliyezungumza kwa lugha ya Kiingereza.
“Kwa nini jamani wasituache wakati Bongo tumepazoea, tumetengeneza fedha nyingi wangetuacha tu kwanza tumeingia kihalali,” alisikika mmoja wa makahaba hao aliyezungumza kwa lugha ya Kiingereza.
Makahaba hao walikamilisha taratibu zote za kusafiri chini ya maofisa wa
uhamiaji kisha wakaondoka na ndege ya Shirika la Qatar saa 12
jioni.Singh alitiwa hatiani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele
ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka baada ya kukiri kosa lililokuwa
linamkabili la kuwaingiza nchini wasichana hao, ambapo aliwatumikisha
kazi ngumu na biashara ya ukahaba kwa lengo la kujipatia fedha.
Mahakama
ilimpa adhabu ya kulipa faini kila kosa Sh milioni tano hivyo kwa
makosa matatu alitakiwa kulipa Sh milioni 15 na magari yake matatu
yalitaifishwa na Serikali.Pia mahakama ilimtaka kuwalipa wasichana hao
22 mishahara yao na endapo mshtakiwa angeshindwa kulipa faini angekwenda
jela miaka 10.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment