tiko
tiko
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Shija Ntelezu, ameungana na baadhi ya wana CCM wengine kumuomba Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, ajitokeze kutangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Ntelezu alisema kwa niaba ya
wana Kishapu wenzake anamuomba Lowassa baada ya kumaliza adhabu
aliyokuwa akitumikia yeye na wenzake watano ni wakati mwafaka hivi sasa
wa kutangaza rasmi nia yake kugombea nafasi hiyo ili ampokee kijiti Rais
Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti
huyo alisema kwa kadri anavyomfahamu Lowassa ni mmoja wa viongozi
wachapa kazi wazuri hapa nchini na mwenye uwezo wa kutoa maamuzi magumu
yanapohitajika kutolewa na kwamba ndiye kwa sasa anayeweza kumrithi Rais
Kikwete na kuendeleza kasi ya kusukuma kasi ya maendeleo
aliyoyaanzisha.
Alisema
wakati taifa likielekea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka
huu ni muhimu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikawa makini kuhakikisha
kinamteuwa mgombea mwenye uwezo wa kukabiliana na wagombea wengine
kutoka vyama vya upinzani.
“Sisi
Kishapu tunaamini iwapo CCM itamsimamisha mgombea jasiri mwenye uzoefu
wa kiuongozi ambaye pia ana historia nzuri ya uchapaji kazi hapa nchini
ambaye haitokuwa kazi kubwa kumnadi kwa wapiga kura nafikiri Lowassa
anatosha kwa nafasi hiyo hivi sasa, yapo mambo mengi makubwa aliyafanya
wakati wa uongozi wake,”
“Utumishi
wa Lowassa unafahamika hapa nchini kuanzia ndani ya chama hadi
Serikalini, kwa sisi wa Shinyanga tunamfahamu zaidi maana aliwahi kuwa
mtendaji wetu enzi ya TANU, lakini kikubwa tunachokikumbuka ni jinsi
alivyowezesha kutufanikishia mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa
Victoria,” alieleza Ntelezu.
Alisema
ni muhimu vikao mbalimbali vya uteuzi ndani ya CCM vikawa makini katika
kufikia maamuzi yake na wajumbe wake wasikubali kuyumbishwa na maneno
ya watu wasiokitakia mema chama hicho na kwamba kimchunguze kwa umakini
kila mgombea aliyejitokeza bila ya kumpaka sifa mbaya za uongo.
Mwenyekiti
huyo alifafanua kuwa ushauri wao wa kumtaka Lowassa agombee nafasi hiyo
ya urais si kwamba wana CCM wengine waliojitokeza hawana sifa hizo,
bali ni muhimu kumpa kipaumbele mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kiutendaji
ndani ya serikali na chama.
“Ushauri
wetu usichukuliwe kwamba wana CCM wengine waliokwisha tangaza nia
hawafai au hawana uwezo na hakuna anayewalaumu, maana ni haki yao ya
kikatiba, lakini tunaangalia ni yupi miongoni mwao mwenye uwezo zaidi
atakayeweza kukivusha chama chetu kwa urahisi kwenye uchaguzi mkuu
ujao,” alieleza.
Akifafanua
kuhusu uwezo wa Lowassa Ntelezu alitaja baadhi ya mambo makubwa
aliyoyafanya alipokuwa waziri katika wizara mbalimbali nchini na pale
alipokuwa waziri mkuu na kutaja baadhi ya shughuli kubwa kuwa ni pamoja
na maamuzi ya ujenzi wa sekondari za kata ikiwemo ujenzi wa Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM).
Lowassa
pamoja na makada wengine watano, Frederick Sumaye, William Ngeleja,
January Makamba, Bernard Membe na Stephen Wassira juzi walimaliza rasmi
kifungo cha miezi 12 walichopewa na kamati kuu ya CCM ikiwa ni adhabu ya
kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho na kuanza kampeni za kuwania
urais kabla ya wakati.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment