tiko
tiko
HATUNA budi
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena katika uwanja wetu
maridhawa wa kupeana darasa la uhusiano. Siku zote ukikubali kupokea na
kufanyia kazi yale tunayopeana kila Jumamosi kupitia safu hii.
Leo
ni siku ya wapendanao (valentine‘s day). Ni vyema basi ukaitumia siku
hii kutafakari na umpendaye. Kumpa zawadi, kutafuta sehemu tulivu na
kujadili uhusiano wenu.Ifanye siku hii kuwa mwanga mzuri wa penzi lenu.
Kama mligombana, tumieni nafasi hii kuombana msamaha na kuanza upya
safari yenu. Usikubali kuendelea kuishi katika penzi ambalo halina
mwanga wa mbeleni.
Kwa siku hii ya leo, si lazima uoneshe upendo kwa mpenzi wako pekee,
unaweza pia kuonesha upendo kwa baba, mama, rafiki na watu
wanaokuzunguka. Watakie sherehe njema ya valentine.
Kwa wale tuliokuwa pamoja wiki iliyopita, tulikuwa na mada yetu
iliyohusu mke wa mtu kuwa mke wa watu. Nilieleza namna ambavyo mke wa
mtu anavyoweza kuangukia katika dmbwi la kuwa mke wa watu kwa sababu ya
kukosa umakini.
Anashindwa kujua kwamba kama mke wa mtu anapaswa aishi vipi na ndugu,
jamaa na marafiki ili asitoe mwanya wa watu kumfanya mke wa
watu.Tumalizie mada hii kwa kutazama mazingira na vichocheo
vinavyowasababisha mke wa mtu ageuke kuwa mke wa watu. Mbali na kujua
vichocheo hivyo, pia tutapata kujua mbinu mbalimbali za kuepukana na
tatizo hili:
UMBALI
Unapokuwa umeolewa moja kwa moja utakutana na mashemeji utakutana na marafiki wa kiume kama vile ulivyokuwa hujaolewa. Suala la msingi hapa ni mabadiliko. Unatakiwa kubadilika ili usiweze kutoa mwanya wa vishawishi.

Kama mtu ni shemeji yako, muwekee mipaka yake. Usikae naye kama vile
unavyokaa na mumeo. Hata kama yeye ataleta ukaribu, wewe ndiyo unatakiwa
kuweka mipaka. Ukiruhusu akukaribie, utarusu akushike na baadaye
anaweza kufikia hatua ya kula tunda analokula kaka yake.
Epuka mazoea yasiyo kuwa na tija. Mazoea ndiyo yale ndiyo yanaletaka
‘shemeji shemeji huku mwazima taa.’Utani unaanzaga taratibutaratibu,
unaota mizizi na baadaye mnafanya kweli. Mtu ambaye si mume wako,
hakikisha hakukaribii. Mpe salamu, zungumza naye lakini asiwe karibu
kupindukia.
KIPAUMBELE
Kama binadamu, wanawake nao wana matamanio. Anaweza kuvutiwa na kitu fulani kutoka kwa mtu fulani ambacho pengine mumewe hana. Ataanza kwa kuvutiwa, baadaye atataka kuonana naye na mwishoni wanajikuta ni wapenzi.

Mke anayejiheshimu hawezi kumpa kipaumbele mwanaume mwingine yeyote kwa
kigezo chochote. Mumewe ndiyo wa kwanza katika hali yoyote. Hata kama
mwanaume fulani ana fedha kuliko mumewe, ana sifa ya ziada kuliko
mumewe, anapaswa kusema mumewe ndiyo zaidi.
Kamwe hampi kipaumbele mwanaume mwingine. Ukimwambia mwanaume mrefu
mzuri, hata kama mumewe ni mfupi atakwambia mumewe ni mrefu kuliko
wanaume wowote. Hivyo ndivyo inavyotakiwa.
Atakwambia ameridhika na urefu wa mumewe ndiyo alioupendea. Hilo ndilo penzi la dhati.
Atakwambia ameridhika na urefu wa mumewe ndiyo alioupendea. Hilo ndilo penzi la dhati.
KUTOTOA SIRI
Mwanamke ambaye hana heshima hutoa siri za ndani. Kama mumewe ana tatizo fulani, analiweka wazi kwa marafiki wa kiume wa mumewe pasipo kujua anatoa mwanya wa kutongozwa. Wanaume wajanja wanasoma udhaifu, wanakutimizia na furaha yako inaendelea kuwepo bila ya mumeo.

Tunza siri. Kama kuna tatizo la faragha, jaribu kuzungumza na mwenzako
ili mtafakari kwa pamoja kuhusu suluhu. Kama ni tatizo linaloweza
kutibika hospitali, nendeni mkapate ushauri wa kitabibu.
Ni matumaini yangu endapo utayazingatia hayo tuliyoyadili, hakikaka
huwezi kuwa mume wa watu bali utakuwa mume wa mtu mmoja ambaye mtaishi
kwa upendo, amani na furaha.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment