tiko
tiko
Vuguvugu la kumuomba kugombea urais aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, linaendelea kupamba moto baada ya wenyeviti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini (ALAT) mkoani Shinyanga kumtaka atangaze rasmi nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa
ombi hilo mbele ya waandishi wa habari juzi mjini Shinyanga kwa niaba
ya wenyeviti wenzake wa halmashauri za wilaya mkoani humo, Mwenyekiti wa
ALAT mkoani Shinyanga, Justin Sheka, alisema wanaamini mtu anayestahili
kupokea kijiti cha urais, Rais Jakaya Kikwete si mwingine bali ni
Lowassa.
Sheka,
alisema yeye na wenyeviti wenzake wa Halmashauri za wilaya mkoani
Shinyanga wanaamini iwapo Lowassa atamrithi Rais Kikwete, ataweza
kuendeleza mipango yote ya maendeleo itakayoachwa na rais anayemaliza
muda wake na kwamba wanaompinga asigombee urais hawaitakii mema nchi
yao.
Alisema
ni wakati mwafaka hivi sasa kwa wana-CCM wote wanaotoka mikoa ya Kanda
ya Ziwa waliotangaza nia au kutaka kutangaza kugombea nafasi ya urais
waunganishe nguvu zao kwa Lowassa ambaye ndiye mwenye uwezo wa kufanya
mambo makubwa kutokana na ujasiri alionao wa kuchukua maamuzi magumu
kila panapostahili.
“Sisi
tunaamini mtu ambaye anastahili kuvaa viatu vya Rais Kikwete kwa hivi
sasa ni Lowassa, waswahili walisema, Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake
mpeni, huyu bwana pamoja na mapungufu ya hapa na pale ya kibinadamu,
lakini bado ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kuitumikia nchi hii
akilinganishwa na wengine,” alisema.
“Uzoefu
wa Lowassa unafahamika na Watanzania wengi hasa wale wa mikoa ya Kanda
ya Ziwa, yapo mambo mengi aliyoyafanya akiwa waziri mkuu hasa katika
sekta ya elimu, kabla ya mwaka 2007, hatukuwa na sekondari nyingi,
lakini baada ya kauli yake ya ujenzi wa sekondari za kata tumepata shule
nyingi za kutosha,” alieleza Sheka.
Sheka
ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga, alisema wapo baadhi ya Watanzania wanaopinga na kudai Lowassa
hastahili kukabidhiwa urais wa nchi hii kwa vile tu wanachuki binafsi
dhidi yake au hawaitakii mema Tanzania.
“Sisi
tumekaa na kutafakari sana huku tukiwachambua wana CCM wote ambao
tayari wametangaza nia ya kutaka kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu
utakaofanyika nchini kote Oktoba 25, mwaka huu, tumebaini kati yao mtu
mwenye uzoefu na uwezo mkubwa ni Lowassa,”
“Hatusemi
wengine hawafai, lakini tunafikiri suala la uzoefu wa kutosha wa
kiuongozi ni jambo muhimu, pia mgombea lazima awe na sifa ya ziada
tunataka rais ajaye awe ni yule mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu
pale inapohitajika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake, na mtu huyo
si mwingine bali Lowassa,”
“Kwa
upande wetu wenyeviti wa ALAT kutoka halmashauri za wilaya mkoani
Shinyanga tunamuomba mheshimiwa Lowassa ambaye mpaka sasa hatujasikia
kauli yake rasmi atamke wazi kwamba atagombea urais na sisi tuko nyuma
yake tutamuunga mkono kwa nguvu zote,”alieleza Sheka.
“Binafsi
naamini wana CCM wote waliotangaza nia wanafaa, lakini lazima tuangalie
miongoni mwao ni mtu gani mwenye uzoefu mkubwa wa kiuongozi hasa upande
wa utawala, mwenye maamuzi ya papo kwa papo kwa masilahi ya taifa lake,
na hawa wengi wanaweza kupewa nyadhifa nyingine ili kuunda serikali
imara,” alisema Sheka.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment