tiko
tiko
Wakati CCM kikijiandaa kuanza mchakato wa kupitisha jina la mgombea wake wa nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, imeelezwa kwamba hali si shwari ndani ya chama hicho kutokana na kile kinachodaiwa, mkakati wa baadhi ya viongozi kubeba na kukumbatia watu wao kwa lengo la kulinda masilahi binafsi.
Chanzo
chetu cha kuaminika kutoka ndani ya CCM kimeeleza kuwa joto kubwa
linazidi kufukuta kuelekea mchakato wa kupata jina la mgombea kutokana
na tabia ya baadhi ya viongozi kupigia debe majina na watu wanaoamini
wakishinda watanufaika nao kwa kulinda masilahi binafsi.
Akizungumza
na Mpekuzi jana, kwa sharti la kutoandikwa jina, mmoja wa makada
maarufu wa chama hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
ya CCM ( NEC-CCM), alisema kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa vigogo wa
chama hicho katika kupata jina na mgombea urais hali ambayo alisema ina
kila dalili za kusambaratisha chama hicho.
“Kuna
tatizo katika kupata jina, tena ni tatizo kubwa, tatizo hili lipo kwa
baadhi ya viongozi wa chama chetu kila mmoja anatembea na jina la mtu
wake mfukoni. Wanahangaika kujipitisha huku na kule kwa visingizio
mbalimbali huku mkono mwingine wanapitisha ajenda za kunadi watu wao.
Hatutakubaliana na hili! Wana-CCM waachwe waamue! Sio kuleteana majina kwa ujanja ujanja hapa,” alilalamika kada huyo na kuongeza;
"Hata Pinda (Waziri Mizengo Pinda) juzi akiwa Iringa, ameonya tabia ya viongozi kutaka kuwachaguliwa wananchi viongozi...Pinda hakutoa kauli hiyo hewani, bali anajua kinachofanyika."
"Hata Pinda (Waziri Mizengo Pinda) juzi akiwa Iringa, ameonya tabia ya viongozi kutaka kuwachaguliwa wananchi viongozi...Pinda hakutoa kauli hiyo hewani, bali anajua kinachofanyika."
Alionya
kwamba mitazamo tofauti ya vigogo hao kubeba watu wao imesababisha
mpasuko mkubwa ndani ya chama na ili kuokoa hilo, busara kubwa
inahitajika.
"Wanafikiri
hatujui, kila mmoja ana mtu wake wanahangaika usiku na mchana, sisi
tunawasubiri wakifanya kosa katika hili wataona matokeo yake, CCM
itameguka vipande vipande.
Kwa tabia hii, wallah CCM inahesabu siku!” Alidai kada huyo na kuongeza;
“Tunaambiwa
baadhi ya vigogo walibeba hadi majina ya baadhi ya waliotimuliwa kwenye
Escrow. Wakahaha sana kupima upepo na kunadi kiujanja ujanja, eti wawe
wagombea wa chama. Haya mambo, sielewi chama chetu kinakwenda wapi?
"Tunafika mahali watu wamejengeka hofu isiyokuwa na maana, wanachukia na kuogopa wengine bila sababu endapo watashika madaraka,” alisema.
Alifafanua
zaidi kwamba tatizo lingine kubwa linalotishia kuathiri mchakato huo ni
kile alichoita, hofu ya ovyo ya baadhi ya vigogo, kuogopa watu fulani
wakishika madaraka.
“Leo
hii watu wanashindwa kutenda haki kwa kuhofia masilahi yao.
Wanalazimisha kubeba hata wasiobebeka. Nini hii? Kupata mgombea wa chama
si jukumu la kifamilia au kikundi fulani! Hii si kazi ya familia moja
ama mbili, hapana!
"Mgombea
asipatikane kwa kupendezesha au kulinda masilahi ya watu. Tunatafuta
mgombea ambaye Mungu akimvusha anakuwa rais wa Watanzania wote.
"Tukichanganya
mambo, kwa suala zito kama hili kwa maslahi binafsi, majibu yake
tutapata muda si mrefu, chama kitaumbuka na wengine hatupo tayari
kuumbuka kwa hofu za watu binafsi zisizo na tija kwa chama na taifa kwa
ujumla. Tumekitoa mbali chama hiki,” alionya.
Alisema
CCM ina viongozi wengi wazuri wenye upeo usiotiliwa shaka, hivyo hakuna
sababu ya kumhofia yeyote kwani chama kinatafuta kiongozi wa chama na
Watanzania wote na siyo korokoroni wa kulinda familia moja au kaya.
Kada
huyo alisisitiza kuwa kila mwana-CCM ana haki ya kugombea nafasi yoyote
ndani ya chama bila hofu wala vitisho na wanachama ndio wenye jukumu la
kumkubali au kumkataa kwa misingi ya kidemokrasia.
Alishauri
vikao vyote vya maamuzi ndani ya chama kutenda haki na kupitisha mtu
kwa sifa, uwezo rekodi na maadili yake katika kuwatumikia wananchi.
Alisisitiza
kuwa shughuli ya kupitisha jina la mgombea wa CCM inapaswa kufanywa kwa
tahadhari kubwa na kuomba viongozi wakongwe wa chama hicho wakiwemo
Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, John Malecela, Pius Msekwa na
Aman Karume kusaidia kubaini, kushawishi na baadaye kupitisha majina ya
watu wanaofaa kubeba jukumu hilo.
“Mimi
nashauri tena kwa msisitizo, viongozi watakaosimamia mchakato huu
watende haki. Wafuate kanuni, wazingatie sifa 13 za mgombea urais. Kwa
hili kuna mtu sitaki kumnyima haki yake, lazima nimsifu , huyu ni
Comredy Mangula (Philip-Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara ).
"Kwa
kusimamia haya Mangula ni jasiri na mkweli hana kona kona za kubeba mtu
au watu, wakati baadhi wana majina mifukoni yeye ana sifa na vigezo
mfukoni mwake.”
Kada
huyo alishauri wana-CCM wenye sifa kujitokeza bila woga kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi ikiwemo urais muda utakapofika. Alisisitiza kuwa
haki pekee ndiyo itasaidia kupata mgombea bora anayekubalika na
wanachama na Watanzania wote.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment