tiko
tiko
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja, amewataka baadhi ya viongozi wa chama hicho kuheshimu haki za wanachama na kuacha siasa za kibabe na kibaguzi kwa kuchunga kauli zao.
Pamoja
na hilo, amewataka viongozi hao kutambua hakuna mtu mwenye hatimiliki
ndani ya chama hicho ila kila mwanachama ana haki sawa ya kukipigania na
kukijenga wakati wote.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mgeja alisema kumekuwa na mambo machafu
ambayo yanajitokeza kwa baadhi ya viongozi wa CCM kutuhumiana ovyo
pamoja na kutoa kauli nje ya utaratibu wa chama.
Mgeja
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amewataka viongozi
hao kuiga mfano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa kuwa
kiongozi shamba darasa kwa makada wengine wa chama hicho.
“CCM
kina utaratibu mzuri sana wa kihistoria uliojengwa kwa heshima,
unaoheshimika kwa jamii kwa muda mrefu ndani na nje ya nchi, lakini hivi
sasa heshima hiyo inaanza kuchezewa na kumomonyoka polepole na baadhi
ya viongozi au kikundi ndani ya chama.
“Kikundi
hicho kwa chuki zao binafsi wanaamua kutoa matamko ya mara kwa mara
ambayo sio ya chama wala hayahusiani na vikao vya chama kwa sababu ya
chuki zao binafsi zisizokwisha, chama ni kikao na maazimio, inashangaza
baadhi ya watu wamekuwa wakitoa matamko ambayo siyo maazimio ya vikao,” alisema Mgeja.
Alisema
watu hao ni hatari kwakuwa wamekuwa wakitoa matamko yenye ukakasi,
maudhi na kichefuchefu na kudai kauli hizo zitakigharimu chama, hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
“Nawaomba
hao wanaosema ovyo na kauli za vitisho kwa wana CCM wengine watambue
chama hiki si mali ya viongozi bali ni mali ya wanachama na hakuna
mwenye hatimiliki na CCM.
“Msitulazimishe
tufike mahala kuona chama kilifanya makosa kuwapa dhamana na kuwatwisha
jukumu ambalo hamliwezi, dhamana mliyonayo hailingani na maneno mazito
ambayo mnayatoa yanayowazidi umri,” alisema Mgeja.
Pia
ametoa wito kwa wananchi na wafuasi wa chama hicho kuwapuuza viongozi
na wanachama wanaoongea hovyo nje ya maagizo ya vikao halali.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment