tiko
tiko
Balozi
wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary
Daud”Zembwela”(kushoto)akimkabidhi fedha mmoja wa abiria wa basi
linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano cha
ubungo kwenda Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwalipia
abiria wenzake nauli ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja wa kampuni
hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.Mkazi
wa jijini Dar es Salaam Mudy Seleman(kushoto)akikabidhiwa fedha kwa
ajili ya nauli na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na
Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” wakati wa kuhamasisha wateja wa
kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda
iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar
es Salaam.Baadhi
ya wanafunzi waliokuwa wakisubiria usafiri katika kituo cha mabasi cha
mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania
Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)baada ya kuwalipia nauli wakati wa
kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili
kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo hicho.Meneja
uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akitoa elimu kwa
mmoja wa abiria wa basi liendalo Gongolamboto kutoka kituo cha mabasi
cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam juu ya Promosheni ya
JayMillions.Baadhi
ya abiria wakiwa na watoto wao katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano
ubungo jijini Dar es Salaam, wakifafanuliwa jambo na mfanyakazi wa
Vodacom Tanzania Joyce Mhina kuhusiana na Promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na kampuni hiyo wakati Balozi wa promosheni hiyo alipoenda
kituoni hapo kutoa elimu kuhusiana na promosheni hiyo na kuwalipia
wasafiri wote bure wa daladala nauli kulingana na sehemu wanayo kwenda
ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni
hiyo.Balozi
wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary
Daud”Zembwela”(aliyesimama)akitoa elimu juu ya promosheni hiyo kwa
abiria waliopanda daladala zinazofanya safari za mlandizi kutoka kituo
cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam na aliwalipia
nauli abiria wote bure ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi
kushirikia katika promosheni hiyo.Kondakta
wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha
Mawasiliano ubungo kwenda Kawe jijini Dar es Salaam, Hamis
Omari(kushoto)akikabidhiwa nauli ya abiria wote waliopanda gari lake na
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania
Hilary Daud”Zembwela”(kulia) wakati alipokuwa akihamasisha wateja wa
kampuni hiyo kituoni hapo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama
wameshinda. Ambapo abiria wote waliokuwepo kituoni hapo walilipiwa nauli
kulingana na safari zao.
Jaymillions wa Vodacom awataka watanzania kuchangamkia fursa
- Ahimiza wateja kuangalia kama namba zao zimeshinda kila siku
-Atembelea stendi ya mabasi Ubungo na kumwaga ofa kwa wasafiri
- Ahimiza wateja kuangalia kama namba zao zimeshinda kila siku
-Atembelea stendi ya mabasi Ubungo na kumwaga ofa kwa wasafiri
Dar es Salaam Februari 15,2015: Balozi wa promosheni ya Jaymilioni
inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Hillary
Daud ‘Jay’ mwishoni mwa wiki alikuwa kivutio kwa wananchi wengi
alipotembelea eneo kituo cha mabasi cha Ubungo Mawasiliano na kuwahimiza
wananchi kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maisha yao ambapo
pia alitoa ofa ya kuwalipia nauli wasafiri waliokuwa wamepanda mabasi
kuelekea sehemu mbalimbali za jiji waliokuwa kituono hapo.
Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa wananchi waliokuwa eneo hilo
ambapo baadhi yao walilazimika kuacha shughuli zao kumwangalia balozi
huyo na wengine kuomba kupiga naye picha ikiwemo waliompiga picha kwa
kutumia simu zao zao mkononi.
Bwana Jay alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa wanaotumia mtandao
wa Vodacom wahakikishe kila siku wameangalia kama namba zao zimeshinda
mamilioni ya fedha kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 na aliwataka
wale ambao hawako kwenye mtandao wa Vodacom wajiunge nao ili washiriki
kwenye promosheni hii kubwa iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania
wengi kuwa mamilionea.
“Leo nimewafuata huku kuwapatia ofa na kuwafikishia ujumbe kwa maana
naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia iwapo
namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha kwa ajili
yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni ya fedha
katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa shilingi
milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa shilingi
milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom”.Alisema
Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, aliwahimiza
wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno
JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema
kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544
iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi
300/-
Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi uliopita mteja
mmoja ameishajishindia milioni 100, wateja 2 wamekwishajishindia
milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha jishindia shilingi milioni
moja kila mmoja na maelfu ya wateja wengine tayari wamejishindia muda
wa maongezi.
Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia mamilioni ya fedha kupitia
promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi nyumba ya wageni wilayani
Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia milioni 100. Waliojishindia
milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro Kanumba mkulima kutoka Inyonga
mkoani Rukwa na James Mangu mfanyabiashara kutoka wilayani Magu
Washindi wa milioni moja ni Chiphold Wanjara mjasiriamali wa Kutoka
Mwanza ,Janeth Nganyange wa Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka
Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima
kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara
wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu
mchapishaji kutoka Arusha,Modesta Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho
mkoani Ruvuma na Nobert Minungu mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.
“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo juma hili
inaingia katika wiki ya nne na bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri
watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia
kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno
Jay kwenda namba 15544.”Alisisitiza.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment