tiko
tiko
MTANGAZAJI na
muigizaji wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amezua tafrani
la aina yake baada ya kutinga kwenye baa moja iliyopo maeneo ya
Mwananyamala jijini Dar akiwa nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo Lulu alipoingia alipita katikati na
kwenda katika kaunta ya baa hiyo huku akijitingisha makusudi na
kusababisha wanaume waliokuwa wamekaa kwenye baa hiyo wapige kelele
wakimtaka aondoke.
“Hii sasa ni sifa haiwezekani atuvalie kigauni kifupi namna hii,
akibakwa atasemaje? Hatukubali, bora ingekuwa usiku, tumwambie mwenye
baa kama anataka amtoe huyu au sisi tuondoke, hata kama tuko baa lakini
tunajieheshimu,” alisikika mmoja wa wanaume hao.
“Huu ujinga bwana sisi tunajiheshimu, hawezi kuvaa hivi tena inaonesha
hana hata kufuri, bora niondoke eneo hili,” alisikika mwanaumwe mwingine
na kuondoka zake.Hata hivyo, meneja wa baa hiyo aliwasihi watu kubaki
na kumvumilia lakini wengi wao waliamua kuondoka kwa hasira.
...Akiwa kwenye pozi.
Waandishi wetu walipomuuliza sababu ya kufika pale na kiguo hicho
alisema kuwa alifika kwa mambo yake muhimu na kukutana na rafiki zake
Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha hivyo kama wateja wengine
wamemsusuia, watajijua.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment