tiko
tiko
MSANII wa sinema za Kibongo, Manaiki
Sanga ametangaza nia ya kutaka kwenda kupeleka posa kwa staa wa sinema,
Jacqueline Wolper, kwa madai kuwa anampenda sana.Akizungumza na
mwandishi wetu, Manaiki alisema hapa Bongo wanaume wengi hawajui
wanawake wazuri lakini kwa upande wake ameona uzuri wa Wolper ni pambo
la moyo wake, atapeleka barua nyumbani kwao.
“Ni maoni yangu, mwaka huu mwanzoni napeleka posa kwa wazazi wa Wolper naamini ndiye mwanamke ambaye anafaa kuwa mke wangu labda tu tatizo kubwa liwe kwake lakini siwezi kubadilisha nia yangu,” alisema Manaiki ambaye anatarajia kutoa filamu yake inayoitwa AMKA aliyowashirikisha mastaa kibao kama Kajala, Majuto, Hemed, Mlela na wengine kibao.
tiko
tiko
Post a Comment