tiko
tiko
DIVA wa filamu Bongo, Wastara Juma amelia na mastaa wenzake wa filamu kususia kisomo cha marehemu mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita
aliandaa kisomo cha kumuenzi marehemu Sajuki ambapo dua ilianzia kwenye
makaburi ya Kisutu alipozikwa na kumalizika nyumbani kwake maeneo ya
Tabata Barakuda jijini Dar.
Akipiga stori na paparazi wetu mwanadada
huyo ambaye alionekana akiangua kilio kizito kwenye kaburi la mumewe
huyo alisema, kamwe kwenye maisha yake hataacha kumlilia Sajuki sababu
ndiye mwanaume pekee aliyemuonesha upendo wa kweli na kujivunia thamani
yake kama mwanamke anayeishi kwenye ndoa.
Kuhusu mastaa kususia kisomo hicho, Wastara alisema;
“Hilo nililijua mapema sababu hawa wasanii wenzangu mambo ya maana hawapendi kabisa, hapa ungewaalika kwenye sherehe yenye pombe wangefika kwa wingi lakini suala la dua wameona tabu sana kuja, nimeshazoea siwezi kulipa kisasi kwa yeyote yule nitajumuika nao kama kawaida japo jambo hili limenikwaza mno.”

Baadhi ya mastaa waliofika katika kisomo hicho ni Davina, Sandra, Vanitha, Frank, Nisha na Mtitu.
tiko
tiko
Post a Comment