tiko
tiko
Kama ulidhani Frank alichukulia poa
baada ya kuharibiwa safari yake ya kwenda kuigiza filamu jijini London,
Uingereza mwaka jana, basi tambua kwamba alikuwa na nyongo ambayo mwaka
huu ameamua kuitema.
Akizungumza na Gazeti la Mwananchi,
muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Mohamed Mwikongi, alisema
suala hilo lilimfanya ajisikie vibaya sambamba na kumjengea picha mbaya
na hasa katika umoja uliokuwepo katika klabu ya Bongo Movie na
aliyemfanyia hayo alikuwa mmoja wa wanachama.
“Bongo Movie tuko vizuri, sitaki
kujilinganisha na Bongo Fleva, ishu ndogo tu ya kutokujitambua ndiyo
inaharibu. Chembe chembe za ubinafsi ndiyo zilizotawala, zinashindwa
kutuweka pamoja, yamesalia majungu basi,” alianza kwa kusema mwigizaji
huyo aliyedumu kwenye tasnia kwa miaka 15 sasa. Alisema baada ya kupata
taarifa kuhusu safari yake, alijipanga na kufurahia sana, lakini
alishtushwa na kukatika kwa mawasiliano baina yake na kampuni ya Didas
Entertainment ambayo alifanya nayo makubaliano.
“Kuhusiana na ile safari yangu ya
London, nilifurahi sana kupata nafasi hiyo kwa sababu sikuwahi kufika
nilikuwa naisikia tu, sasa unapoona mtu anaingia katikati mazingira
yanakuwa ni tofauti kidogo katika mambo binafsi ambayo mimi nashindwa
kuelewa,” alisema na kuongeza:
“Sisi wasanii upande wa wasambazaji
wanatugawa na sisi wenyewe tunajigawa, ukija upande wa serikali
imetugawa, wananchi nao wanatugawa kutokana na sisi kutokuwa na msimamo
hasa wa kimaendeleo ya kisanaa.”
Frank anasema katika suala kama hilo
msanii anapopata kazi, halafu mwingine anamharibia ni tatizo kubwa sana
ambalo hurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi.
“Mtu anaposema huyu hafai, mimi ndiyo
nafaa tayari hilo ni tatizo. Ina maana sisi wenyewe tumejigawa, kwa hiyo
wasanii hatuna msimamo, mtazamo, mshikamano na umoja ila tumejawa na
unafiki ambao umetutawala na ndiyo ambao tunaona ndiyo sehemu ya maisha,
lakini unaturudisha nyuma” alisema na kuongeza;
“leo hii mimi hata kama nikipata nyumba
nikichukua mkopo benki, ikija kunifuata kwa ajili ya marejesho kama sina
nikanyang’anywa nyumba wasanii watanicheka na siyo kushikamana na
kukusaidia kuikomboa ile nyumba.”
Frank alisema klabu ya Bongo movie bado
ina matatizo ambayo yanahitaji kupata kiongozi mzuri wa kuyatatua,
lakini kwa sasa haina kiongozi waliokuwapo walijiuzulu.
“Ili tuweze kukaa kwenye mstari
unaonyooka katika hali hii inatakiwa wasanii tuwe pamoja, katika suala
la kimtazamo, kujitambua na kisheria ili kujifahamu wapi tunakwenda na
tunafikia kwa kiasi gani maendeleo ambayo tunakuwa nayo, tukishayakamata
hayo nina imani kwamba kila mmoja anaweza kuwa na haki katika upande
wake na nafasi ya kumwambia mwenzake wapi tumekosea na tukaweza
kusaidiana,” alisema Frank. Mwezi Aprili mwaka jana mwigizaji Issa Musa
“Cloud 112” alidaiwa kumfanyia fitina na majungu Frank katika kazi ya
kwenda kuigiza filamu nchini Uingereza na badala yake alikwenda yeye.
Kampuni iliyoandaa filamu hiyo Didas
Entertainment, iliweka ushahidi wote hadharani Oktoba mwaka jana,
ikiwamo vielelezo vya ujumbe uliotumwa na Cloud 112 zilizokuwa
zikimwelezea Frank kama msanii asiyefaa kupata nafasi hiyo.
Licha ya vielelezo hivyo, Cloud 112 mpaka sasa bado anakana tuhuma hizo na kudai kwamba makubaliano yake yaliyokuwa ni tofauti.
Sikumfitini Frank, yule mtu alinifuata
mwenyewe kwa makubaliano ya mdomo kuwa nikacheze filamu. Sikuwa peke
yangu, tuliongozana na Monalisa na Riyama, tatizo ni la huyo
aliyenipeleka kule, nilifanya mambo kwa mazoea,” alisema.
na ndiyo sababu aliamua kusambaza uongo dhidi yangu,” alisema.
tiko
tiko
Post a Comment