tiko
tiko
Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea hii leo kwa michezo kumi iliyopigwa kwenye viwanja kadhaa nchini humo.
Ukiachana
na mchezo wa Manchester United uliofanyika mapema ambapo mashetani hao
wekundu walishikwa shati na Stoke City , mwanzo wa mwaka haukuwa mzuri
kwa timu kubwa baada ya timu mbili za London ambazo ni Chelsea na
Arsenal kufungwa kwenye michezo yake .
Chelsea
wakiwa wageni wa Tottenham Hotspurs huko White Hart Lane walipoteza
mchezo wao kwa kufungwa 5-3 katika mchezo ambao ulijaa magoli tangu
mwanzo .
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Hispania Diego Costa alikuwa wa kwanza kuifungia timu
yake mapema kwenye dakika 18 baada ya kumalizia mpira wa shuti uliopigwa
na Oscar na kugonga mwamba .
Spurs
walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 30 mfungaji akiwa mshambuliaji
kijana Harry Kane aliyefunga kwa shuti la umbali wa karibu mita 25 baada
ya kumpita Oscar . Baada ya Hapo Spurs walipata bao la pili kupitia kwa
beki wa kushoto Danny Rose ambaye alimalizia mpira wa Nacer Chadli
uliogonga mwamba .
Winger
Andros Townsend alifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki
Gary Cahill kumchezea vibaya Danny Rose , Spurs walipata bao la nne
kupitia kwa Harry Kane kabla ya kumalizia karamu kwa bao safi la Nacer
Chadli .
Mabao
mengine ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard na John Terry . Mara ya
mwisho kwa Chelsea kufungwa idadi kubwa ya mabao kwenye ligi kuu ya
England ilikuwa mwaka 1991 ambapo walifungwa na Nottingham Forest 7-0.
Arsenal
wakiwa kwenye uwanja wa St Mary’s walikubali kipigo cha 2-0 mbele ya
Southampton huku mabao yote mawili yakifungwa kutokana na makosa ya
kizembe ya kipa Wojciech Szczesny. Wafungaji wa Saints kwenye mchezo huo
walikuwa Sadio Mane na Dusan Tadic .
Katika
michezo mingine Manchester City walishinda mchezo wao dhidi ya
Sunderland kwa 3-2 , Liverpool na Leicester City wakitoka sare ya 2-2 ,
Newcastle na Burnley nao walifunga 3-3 huku West Ham United na West Brom
wakiendeleza mfululizo wa sare baada ya kufungana 1-1 .
Matokeo
haya yamewafanya Chelsea kupunguzwa kasi baada ya Manchester City
kuwafikia kwa kutimiza pointi 46 huku Southampton wakiwapumulia
Manchester United baada ya kupunguza tofauti ya pointi baina ya timu
hizo ambayo kwa sasa itakuwa pointi moja .
Jumla ya mabao 34 yamefungwa kwenye michezo 10 iliyopigwa leo ukiwa wastani wa angalau mabao matatu kwenye kila mechi moja .
tiko
tiko
Post a Comment